Nghwirwa amemtaka rais huyo mpya kuleta mabadiliko ya uchumi wa nchi
kupitia ilani ya chama cha ACT-Wazalendo kwa kuzingatia uzalendo wa
kutumia vizuri rasilimali za taifa.
Akimakabidhi ilani ya chama hicho, Mghwira amesema kuwa ilani hiyo
ilizingatia usawa wa kijinsia kuwatengeneza benki za wakulima, kuweka
miiko ya uongozi kwa kuzingatia uadilifu.
Wagombea wengine waliohudhuria ni Chief Lutalosa Yemba wa ADC, Fahmi
Dovutwa wa UPDP, Macmillan Lyimo wa TLP, Janken Kasambala wa RNA.
Wasiohudhuria ni Hashimu Rungwe wa Chaumma na Edward Lowassa wa Chadema.
Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo Olengurumwa |
Aidha pia Asasi mbalimbali za kiraia (AZAKI) zimemtaka Rais Mteule, John
Magufuli kuhakikisha analeta Katiba Mpya ili kubadilisha maendeleo ya
nchi na kuondoa matatizo mbalimbali yanayotokana na mfumo mbovu wa
katiba ya sasa.
Asasi hizo zinazojihusisha na masuala mbalimbali
ya kisheria, kijamii, kisiasa na utamaduni zimesema hayo katika mjadala
uliofanyika katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam,
uliozungumzia mambo ambayo Asasi za kiraia zinategemea kuyaona katika
uongozi wa serikali mpya.
Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo
Olengurumwa amesema serikali mpya ni vyema ikaheshimu haki za binadamu
ambazo ni nguzo kubwa katika utawala wa sheria.
“Tunahitaji kuiona Tanzania ikiheshimu haki za binadamu na amri za
kikatiba hivyo katiba mpya ndio itakayosimamia misingi yote hiyo katika
usawa,” anasema Olengurumwa.
Olengurumwa ambaye ndiye mwanzilishi wa mjadala huo amesema mambo
mengine ambayo Asasi za kiraia inatarajia kuona ni mgawanyo mzuri wa
kazi kwa viongozi ili kuongeza ufanisi kwa kila uongozi ufanye kazi
katika kitengo husika.
Kuwepo kwa kasi ya uwazi na kasi ya uwajibikaji wa serikali
Olengurumwa analizungumzia kuwa ni jambo linalowaumiza sana wananchi
kutokana na rushwa zinazopitiliza kwa viongozi wasio wawajibikaji.
Ilani hizo za asasi za kiraia zenye ujumla wa ilani nane ambazo
nyengine ni pamoja na, usawa wa kijinsia, usimamizi wa maendeleo,
kukubalika na kushirikishwa kwa asasi za kiraia pamoja na upatikanaji wa
huduma muhimu za kijamii.
Olengurumwa amesema asasi za kiraia ni wadau muhimu sana katika
maendeleo ya nchi yeyote wakiwa wanafanyakazi kwa maslahi ya umma na
kusema kuwa tunaitaka serikali mpya iangalie asasi hizi na itambue kuwa
zinamchangi mkubwa katika maendeleo.
No comments:
Post a Comment