TTCL

EQUITY

Sunday, October 11, 2015

MUDA ULIOBAKI, MIDAALO KWA WAGOMBEA NI MUHIMU

 

 By Kevin Lameck
Binafsi nitumie nafasi hii kupongeza sana kilichofanyika mkoani Iringa siku ya leo.
Ulikuwa ni mdahalo uliowakutanisha wagombea ubunge jimbo la Iringa mjini na hili limefanywa na KLABU ya waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC) kama waandaaji ndani ya ukumbi wa Highlands mjini Iringa.

Ni jambo la kheri na la kupongezwa sana maana limekua na manufaa kwa wale waliokua na dhamira ya kweli kwa kufuatilia mdahalo huo kama wapenda maendeleo wa jimbo hili la Iringa Mjini lakini pia kwa wale wagombea wenye nia ya kweli katika maendeleo kwa wana iringa maana wamepata nafasi ya kuzungumza na wana Iirnga moja kwa moja lakini kupitia redio za hapa Iringa.

IPC kama klabu ya waandishi wa habari pia wamefanya jambo jema na kubwa pia kwa wakazi wa Iringa na jambo hili bila shaka ni la kupongezwa na la kuigwa na klabu nyingine za waandishi wa habari nchini Tanzania.

Kushiriki siasa ni wajibu wa kila binadamu mwenye akili timamu, sababu siasa ndizo zinazotupatia viongozi (wazuri na wabaya) na hawa wana athari za moja kwa moja kwa maisha yetu ya kila siku.

Wakati wa Tz tupo katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, ni muhimu sana haswaa nyie mashabiki wa siasa, siasa zetu zijikite kwenye Misingi‬ na ‪‎Maswala‬ , na sio siasa za kishabiki tu bila kupima na kuchambua kwa kina ajenda walizobeba hao tunaowashabikia, na kwa nini tunawashabikia. 

Tupunguze mihemko ya kisiasa , ushabiki usio na tija, tujifunze kuhoji na kupima (uchambuzi) ambao ndo utakuwa msingi wa maamuzi yetu, kuliko kubakia tu kuwa mtaji wa wanasiasa.
Masikitiko yangu ni kwa vijana ambao ni wasomi lakini hawatumii usomi wao kuchambua na kupima, wameamua kuwa mashabiki.

Nimegundua vijana wengi sasa wameamka kisiasa tofauti na siku za nyuma. safari hii kila kona utawakuta vijana wanadiscus siasa huku wakijaribu kukosoa serikali iliyopo madarakani na wengi wao wakiwa na hamu na 25 october, hili ni jambo la kutia moyo sana. 

Tatizo nililoligundua n kuwa ushabiki umekuwa mwongozo wa vijana wengi, hawaanalyze sifa za kiongozi wanaemtaka na wengi wanafata mkumbo. They do so because the mass is doing. USHAURI WANGU, vijana wajikite kwenye kupambanua aina ya kiongozi wanayemtaka, atakae waongoza kwenye kupata maendeleo, na mengine mengi. 

Sioni haya kutamka katika msimu wa uchaguzi wa mwaka huu ‘ushabiki’ unanuka na kuranda kama rushwa inavyobembea nchini. Huu ni msimu wa tano wa uchaguzi wa vyama vingi vya siasa (1995-2015) uliotanguliwa na misimu minne iliyopita ya kutokuwa na ushabiki mpana na hatari kama huu wa leo. Kulikoni? 

Ushabiki wa msimu wa mwaka huu, umewakumba hata baadhi ya wagombea, viongozi wa siasa na hata waandishi wa habari kama si vyombo vya habari.
Kwa desturi, ushabiki hufanywa na wenye vyama vyao vya siasa. Waandishi au vyombo vya habari vinapomshabikia mgombea maana yake ni nini? Ni vema mkanielewesha. 

Hivi ni kweli Watanzania mpo tayari kupoteza maisha yenu, usalama wenu kwa thamani ya ushabiki? Ushabiki una maana gani mbele ya ukweli na hoja? Ukweli na nguvu ya hoja ndizo zana ya kuleta mabadiliko nchini Tanzania. Ushabiki ni zana ya kuvuruga mabadiliko. 

Ni busara na hekima kwa wanaounda na kuusambaza ushabiki huo kuacha kuusanifu kwani matokeo yake ni kuleta ghasia. Ushabiki huo unaweza kuleta sintofahamu wakati wa kupiga kura na kutangaza matokeo ya kupiga kura kwani kila shabiki atajihesabu ni mshindi ilhali si mshindi.

No comments:

Post a Comment