TTCL

EQUITY

Saturday, October 10, 2015

MTANGAZAJI WA KITUO CHA CHANEL TEN AOMBA MSAADA WA KIMATIBABU

Aliyekuwa mfanyakazi wa Africa Media Group Limited - AMGL inayomiliki vituo vya televisheni vya Channel Ten, DTV, CTN, C2C na kituo cha radio cha Magic Fm, bw. Meshack Nzowah ambaye alipata ajali hivi karibuni anaomba msaada wa matibabu nje ya nchi kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye ajali hiyo.
Meshack Nzowah ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili anatakiwa kusafirishwa kwenda India kwa ajili ya matibabu haraka iwezekanavyo, ambapo kiasi cha shilingi milioni 30 zinahitajika.
Kwa mujibu wa kaka wa Meshack, bw. Masoud Suleiman Nzowah tayari Meshack amepatiwa huduma kadhaa akiwa Muhimbili hospitali ikiwemo kufanyiwa upasuaji wa jicho lakini kwa mujibu wa madaktari, anatakiwa matibabu zaidi ya kichwa.
Kwa yeyote atakayeguswa na kutaka kumsaidia Meshack Nzowah anaweza kuweka mchango wake kupitia akaunti namba 2011 000 9584 NMB HOUSE - yenye jina MASOUD NZOWAH ama anaweza kutuma mchango wake kwa tigo pesa kwenye simu namba 0715 30 41 85 au 0713 461627.

No comments:

Post a Comment