Suala la mtoto wa rais kuja kugombea urais lilionekena kama
tatizo na linaendelea kuonekana kama tatizo barani Afrika lakini mambo
si kama hivyo wanavyodhani waafrika wengi.
Mwezi uliopita, waziri mkuu wa Canada ambaye ni mtoto wa Justin
Trudeau aliyekuwa waziri mkuu wa 15, alichaguliwa kuongoza serikali ya
nchi hiyo.
Ingawa hali hiyo si ya kawaida kwenye nchi nyingi duniani, hali hiyo
hiyo iliweza kushuhudiwa nchini Marekani pale ambapo Rais wa awamu ya
sita John Quincy Adams alichaguliwa kuiongoza Marekani wakati baba yake
ndiye aliyekuwa Raisi wa awamu ya pili John Adams.
Hali hiyo hiyo ilijirudia tena kwa Rais wa awamu ya 43 George W.
Bush aliyeongoza vipindi viwili akiwa ni mtoto wa Rais wa Marekani wa
awamu ya 41 aliyeongoza kipindi kimoja tu.
Ukienda barani Asia utakuta baba anamwachia binti yake kuongoza nchi
kama binti wa aliyekuwa Rais wa Korea ya Kusini, Park Chung-hee
aliyemwachia Pak Geu-hye ambaye ni Rais wa sasa wa Korea ya Kusini
aliyechaguliwa kwa uchaguzi wa demokrasia kabisa na kuwa mwanamke wa
kwanza kuingoza nchi hiyo.
Tukirudi barani Afrika tunakutana na hali hiyo hiyo kwa baadhi ya
nchi kama Zanzibar, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Botswana,
Gabon na Togo.
Zanzibar
Abeid Amani Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar. Alipata wadhifa huo baada ya kutokea mapinduzi yaliyosababisha kupinduliwa kwa Sultani wa mwisho wa Sultan Jamshid bin Abdullah January 1964.
Abeid Amani Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar. Alipata wadhifa huo baada ya kutokea mapinduzi yaliyosababisha kupinduliwa kwa Sultani wa mwisho wa Sultan Jamshid bin Abdullah January 1964.
Miezi mitatu baadaye, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzishwa na Karume akawa makamu wa kwanza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Mwalimu Julius Nyerere akiwa Rais.
Jina la Karume lilirejea tena baada ya Amani Abeid, mtoto wa Karume
kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na kuingia madarakani November 8, 2000
hadi November 3, 2010.
Togo
Faure Essozimna Gnassingbe ambaye ni rais wa sasa nchini Togo
alishika wadhifa wa urais baada ya kufariki baba yake Marehemu
Gnassingbé Eyadéma mwaka 2005. Jumuiya za kimataifa zilipinga wadhifa
huo wa kumtangaza kuwa rais wa nchi hiyo hivyo Togo ililazimika kuitisha
uchaguzi wa kidemokrasia mwaka 2009 ambapo alishinda na kuiongoza rasmi
nchi ya Togo kama rais halali wa nchi hiyo.
Mwaka huu ameshinda tena uchaguzi hivyo ataiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine kwa miaka mitano zaidi.
Gabon
Ali Bongo Ondimba, ni mtoto wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo marehemu
Omar Bongo ambaye aliiongoza Gabon tangu mwaka 1967 mpaka alipofariki
2009.
Baada ya kufariki Mzee Omar Bongo mwanae Ali Bongo Ondimba aligombea
nafasi ya Urais kupitia chama cha Gabonese Democratic Party mwaka 2009
ambapo alishinda kwa kura zilizobeba asilimia 42% ya kura zote.
Ali Bongo hana tofauti na baba yake kwani ilipofika mwaka 2010 alituhumiwa kwa kutumia fedha za walipa kodi wananchi wake na kujinunulia jumba la kifahari nchini Ufaransa.
Ali Bongo hana tofauti na baba yake kwani ilipofika mwaka 2010 alituhumiwa kwa kutumia fedha za walipa kodi wananchi wake na kujinunulia jumba la kifahari nchini Ufaransa.
DR Congo
Joseph Kabila, ambaye ndiye Rais wa sasa kuanzia mwaka 2001, alishika
ofisi hiyo siku 10 baada ya kuuawa kwa Baba yake Marehemu
Laurent-Désiré Kabila. Vile vile alichaguliwa kwenye uchaguzi wa mwaka
2006 na kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili mwaka 2011. Kabila
aliyezaliwa miaka ya 1970 ameongoza Congo kwa miaka 18 hadi sasa.
Uhuru Kenyatta ndiye Rais wa nne wa Kenya ambaye ni mtoto wa muasisi
wa taifa hilo marehemu Jomo Kenyatta. Uhuru Kenyatta anayejulikana
kwamba ndiye rais mwenye umri mdogo aliyewahi kuitawala Kenya, aliingia
madarakani mwaka 2013. Rais Kenyatta amesafiri nje ya Kenya mara
nyingi zaidi akimzidi baba yake ambaye aliweza kusafiri mara mbili tu
kwenda nje ya Kenya kwa miaka 15 ya utawala wake.
Botswana
Luteni Ian Khama, rais wa sasa wa nchi hiyo ni mtoto wa wa rais wa
zamani wa nchi hiyo marehemu Seretse Khama. Kutokana na Historia,
familia hii inatoka ukoo wa kifalme wa mzee Sekgoma II na Malkia Tebogo.
Ian alizaliwa tarehe 27 mwezi wa pili mwaka 1953 wakati wazazi wake
wakiwa kizuizini huko Uingereza.
Alishika madaraka ya kuiongoza nchi hiyo mwaka 2008 na vile vile
alifanikiwa kupewa kuongoza miaka mitano ya kwanza baada ya kushinda
uchaguzi wa wabunge na vile vile mwaka 2014 aligombea na kushinda tena.
No comments:
Post a Comment