Mh. Melance E. Kinabo (anayetetea kiti chake cha udiwani) |
Themi
ni miongoni mwa kata zeyenye rasilimali nyingi ikiwemo viwanda na uwanja wa
maonesho ya siku ya wakulima (nane nane), Wakati Jiji la Arusha likitajwa
kushikilia nafasi ya kwanza kwa usafi
kati ya Majiji yote Tanzania kwa mara ya kwanza, Themi nayo imekuwa miongoni
mwa kata zilizo tajwa kuongoza kwa usafi 2013 - 2014 chini yauongozi wa Mh.
Diwani Melance Kinabo, ikishikilia nafasi ya pili ndani ya halmashauri.
Robo
tatu ya wakazi wa Themi sawa na 60% ni wafanyakazi wa viwandani na wengine
waliobaki ni wafanyakazi katika maeneo mbalimbali. mwaka 2008 wafanyakazi wa
kiwanda kilichokuwa kikizalisha matairi bora afrika mashariki walipewa taarifa
ya kusimama kazi kwa madai kuwa kiwanda amepewa mwekezaji, jambo ambalo
liliathiri wakazi wengi wa themi waliokuwa wakitegemea ujira huo kuendesha
maisha yao.
Themi
imebarikiwa kwa kuwa na viwanda vingi ikiwemo ABB, Kilitex, Sunflag, A to Z,
Breweries, Genera tire n.k ambapo hivi sasa vingi vimeuwawa na serikali tawala
baada ya kukabidhi wawekezaji na sasa kugeuka kuwa maskani ya vibaka na wacheza
kamari, na kimojawapo kugeuzwa eneo la kanisa.
Ujio
wa Mh. Melance Kinabo umekuwa ni faraja kubwa kwa Themi, amabapo aliongoza kwa
kipindi cha miezi michache baada ya kuenguliwa kwa madiwani wanne wa chadema waliobainika
kuwa walikuwa wakitumiwa na CCM baada ya kupokea rushwa kwa lengo la kumpitisha
Meya wa Jiji la Arusha kutoka CCM.
Katikati ni Mh. Diwani wa kata ya Themi wakati akikabidhi Solar (umeme wa jua) katika kituo cha Afya Themi |
Mh.
Kinabo katika kipindi kifupi cha uongozi wake amefanikiwa katika maeneo
mbalimbali nayo ni;
Elimu
Mh. Kinabo amefanikiwa kuanzisha mpango maalum wa kusomesha
watoto 2000 wanaotoka katikafamilia duni, kutoka shule za sekondari 10, na
shule za msingi 10.
Na
katika elimu yapo maeneo mawili ambayo ameyashughulikia, ambapo ni shule za
msingi na sekondari.
Shule za msingi
Shule ya msingi Engira mh. Kinabo amefanikiwa kutekeleza robotatu ya ahadi
zake zote ikiwemo,
Uchimbaji
wa kisima cha maji na ufungaji wa pampu ya kupandisha maji, ambapo imepunguza
adha kubwa ya upatikanaji wa maji kwaajili ya mazingira ya shule na mahitaji
kwa wanafunzi.
Ujenzi
na ukarabati wa madarasa mawili, ambapo yamejengwa kisasa zaidi na kugawanywa
mawili kuwa ukumbi wa mikutano na lingine kuwa darasa maalumu la kompyuta.
Kurudisha
umeme wa shule na kufanya baadhi ya shughuli zinazohitaji umeme kufanikiwa,
kutokana na sehemu kubwa ya elimu na maisha ya sasa kutawaliwa na teknolojia.
Ukarabati
wa choo cha matundu manne cha maji jambo ambalo limeifanya shule ya Engira
kuonekana maridadi na haa kuwa vutia wanafunzi.
Aidha
ufaulu wa wanafunzi wa Engira ulipanda kwa 100% 2013-2014, ambapo Mh. Diwani
amekuwa akionesha ushirikiano katika kila hatua hususa kufadhili ziara za
mafunzo mf. Ziara ya kutembelea hifadhi za wanyamapori ikiwemo Ngorongoro.
Shule ya msingi Themi pia Mh. Diwani amefanikiwa kutekeleza machache
ikiwemo,
Ujenzi
wa vyumba viwili vya madarasa, na ununuzi wa mashine maalumu kwa ajili ya watu
wasioona (Vipofu).
Ukarabati
wa madarasa, na utengenezaji mashelfu kwaajili ya kuhifadhi vifaa vya masomo.
Ufaulu
wa wanafunzi umeongezeka na kufikia 100% 2013-2014.
Shule za Sekondari
Shule ya sekondari Themi Mh. Diwani ametekeleza ahadi zake kwa zaidi ya
asilimia 80%.
Ujenzi
wa maabara tatu za kisasa
Upatikanaji
wa eneo jipya la shule
Ukarabati
na ununuzi wa vifaa vya shule ( ikiwemo madawati na viti)
Ujenzi
wa geti na uzio wa shule
Ukamilishwaji
wa ujenzi wa marasa manne ya ghorofa.
Kwa
kiwango hicho mh. Diwani amechochea kusukuma maendeleo makubwa ya shule ya
sekondari Themi, pia amekuwa akiwaombea wanafunzi misaada ya kiamasomo kupitia
wadau mbalimbali, Taasisi za umma na Binafsi, ambapo ongezeko la ufaulu
limekuwa kwa zaidi ya 65%
Shule ya Sekondari Arusha Day umefanyika ukarabati wa ofisi ya waalimu na maabara
mbili, pamoja na ujenzi wa maabara nyingine ya kisasa, ujenzi wa uzio na geti
la shule, pamoja na ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu kwa usalama wa
wanafunzi na raia wengine.
Afya
Uwekwaji
wa sola (umeme wa juwa) kituo cha afya imegharim, Pia kwa juhudi za Mh. Diwani
umefanyika ukarabati wa vyoo na kuvifanya kuwa na miondombinu rafiki kwa
wagonjwa. Uhamasishaji kwa kila familia kujiunga na afya ya jamii tiba kwa kadi
(TIKA) inayogharimu Tsh. 12,000/= kwa mwaka. Aidha kwakutambua umuhim wa jamii
na afya zao, Mh. Diwani amekuwa mstari wa mbele kutete huduma za afya kufanyika
hadi siku ya jumamosi mpangoa ambao kwasasa umeridhiwa, Mh. Amehakikisha huduma
ya mama na motto inakuwa salama na hivyo amekipatia kituo cha Afya Themi
kitanda maalum na cha kisasa kwaajili ya kujifungulia akinamama wajawazito.
VIKUNDI
Vikundi vya akinamama kwa kuanzisha mradi wa akinamama Themi living garden, mradi huu
unawasaidia akinamam wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, aidha umefanyika
mchakato wa upatikanaji wa (12. M) kwaajili ya kuwakopesha vijana, na
akinamama. Katika awamu ya Mh. Kinabo kumekuwa na ongezeko kubwa la uanzishwaji
wa vikundi vya wajasiriamali katika Nyanja mbalimbali mfano vikundi vya sanaa, kuweka
na kukopa n.k (kutoka vikundi 7, hadi kufikia 21).
MIUNDOMBINU
Umefanyika
ukarabati wa ofisi ya Afisa mtendaji kata ya Themi na kurejeshwa umeme uliokuwa
umekatwa kutokana na deni lililokuwepo hapo awali. Pia umefanyika ukarabati wa
barabara za mitaa ya naenane, kambini, barabara ya Biya, kambarage, na
ukarabati wa Barbara ya lami kutoka reline hadi uhasibu, kwa ushirikiano na
kata ya Olorieni Mh. Amefanikiwa kujenga kivuko cha mtaa wa kambarage. Kufunguliwa
na kutumika Barbara ya mount meru kupitia mahakama kuu, iliyokuwa imefunwa kwa
muda mrefu.
HALMASHAURI
Ukuwaji
wa mapato ya halmashauri kutoka 500 Million hadi 1.3 Billion.
Kufanya
ushawishi wa serikali kununua mitambo maalumu kwaajili ya ujenzi wa miundombinu
grader 1, compactor machine 1, na malori 3, kupatikana kwa hati safi baada ya
miaka 5 ya hati zenye mashaka. ununuzi wa gari la wagonjwa (Ambulance), kushawishi
na kutetea Arusha kuingizwa ktk (Master plan) mpango maalumu wa kuendeleza jiji
la Arusha.
Haya
ni miongoni mwa mafanikio ya Mh. Melance Kinabo katika kipindi chake cha
uongozi, hivyo kwa kasi hii, uwezo na uthubutu aliouonesha ni dhahiri
anakilasababu ya kupewa dhamana ya kurejea ili kuendelea kukamilisha mengine
aliyoahidi na kukosa muda wa kutekeleza yote.
Themi
inahitaji kurejesha heshima yake, kata hii inautajiri mwingi na iwapo serikali
itakuwa makini katika kusimamia na kuweka mikakati yake vyema Themi inauwezo
wakutengeneza zaidi ya 65% ya ajira kwa vijana wengi waliopo nchini wasio na
ajira, pia inaweza kuwa kata pekee yenye kuchangia pato kubwa la Halmashauri
kutokana na wingi wa viwanda vyake vilivyo uawa na wawekezaji.
Kwa kuzingatia sifa za uongozi bora Mh. Melance Kinabo ndiye kiongozi mwana harakati na mtetezi wa Themi, kwakua anayoniya, uthubutu, sauti ya umma, msemaji na mtendaji mwaminifu.
Kwa kuzingatia sifa za uongozi bora Mh. Melance Kinabo ndiye kiongozi mwana harakati na mtetezi wa Themi, kwakua anayoniya, uthubutu, sauti ya umma, msemaji na mtendaji mwaminifu.
No comments:
Post a Comment