Polisi
mkoani Arusha walimkamata mwanasiasa huyo pamoja na watu wengine wanne
juzi jioni mara baada ya kuzindua kampeni yake ya kuwania ubunge katika
jimbo hilo kwa awamu ya pili katika Shule ya Msingi Ngarenaro.
Mgombea
ubunge jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Godbless Lema na wenzake wanne wameachiliwa kwa
dhamana jana baada ya kushikiliwa na polisi juzi.
Wakisomewa
mashtaka katika mahakama ya Arusha, Lema amedaiwa kulizima gari lake
wakati wakitokea kwenye mkutano wa kampeni, hali iliyowafanya wafuasi
wake kuanza kulisukuma hivyo kusababisha maandamano pasipo kuwa na
kibali cha polisi. Lema na wenzake wameyakana mashtaka dhidi yao.
Mwanasiasa huyo na wenzake wameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana waliyowekewa.
No comments:
Post a Comment