Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisani fomu ya udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea huyo. zoezi hili limefanyika jioni ya leo Juni 27, 2015 kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar. ambapo kwa wilaya ya Kinondoni amepata udhamini wa wanaCCM 95, 251 na kufanya jumla kuu kuwa 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini Mh. Lowassa.
Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akiwasalimia wananchi wake.
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan akisalimia wananchi wake.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akiwasalimia wanaCCM wa Wilaya ya Ilala, Jijini Dar.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assah Simba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa kuwasalimia na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Ilala
waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania
kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 27, 2015.
Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Robert Kerenge akikabidhi fomu za Wadhamini kwa Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa leo Juni 27, 2015. Jumla ya WanaCCM 72, 100 wa Wilaya ya Temeke
Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa
Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba
25, 2015.
No comments:
Post a Comment