Kama umepatwa na majanga haya ya kuibiwa kifaa chako inaweza kuwa simu au hata kompyuta yako, pole. Lakini kama hayajakufika kumbuka yanaweza kukukuta, hivyo basi ni vyema kujua nini utafanya kama yakitokea.
Wengi
wakipoteza au kuibiwa vifaa vyao hukimbilia kubadili neno siri
(password) za mitandao yao ya kijamii hasa facebook, lakini kwa nini
ufanye hayo yote wakati kuna njia rahisi kabisa?. Mtandao wa kijamii wa
Facebook unaweza tumiwa vibaya na mtu ambae amepata simu yako pasopo na
kibali (ameiba) na kukuweka katika matatizo.
Haitajalisha
ulikua unatumia simu gani kama ni Android, Windows, iPhone basi unaweza
Log out Facebook kwa kutumia njia hii ifuatayo.
MUHIMU: Njia
hii inaweza fanyika kwa kutumia kompyuta tuu na sio simu. Kama hutaki
meseji,picha na mambo yako mengine muhimu Facebook kuonwa na mtu
mwingine ambae ana simu yako basi futa yafuatayo
- Kwa kutumia kompyuta ingia katika akaunti yako ya Facebook
- Click kwenye Menyu ya kushuka na kisha chagua ‘Settings’
- Ukiwa katika ‘settings‘ angalia upande wa kushoto na kisha click ‘Mobile’
- Baada ya ku click utatokea ukurasa ukikuuliza kama umepoteza simu yako yaani Lost your phone? bofya link hiyo
- Itakuuliza u ‘log out‘ katika simu yako iliyoibiwa/iliyopotea.
No comments:
Post a Comment