Wahusika wa masuala ya usalama wamesema huenda ni chuki na hasira tu za mtu binafsi zilizofanya kutokea kwa tukio hilo, watu walikuwa wanasali Emanuel AME Church, Charleston Marekani, akatokea mtu mmoja akafyatua risasi kwa watu waliokuwa wanasali.
Watu tisa wamefariki, bado hakuna taarifa rasmi kuhusu idadi ya watu wote waliokuwemo ndani ya Kanisa hilo… Mtu anayetuhumiwa kwa mauaji hayo ni kijana ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 hivi.
Tukio limetokea June 18 2015, Jimbo la Carolina Marekani.
Kanisa la Emanuel AME Church ni Kanisa la Kihistoria ambalo lilijengwa mwaka 1816 ambapo watu wengi wanaosali humo mpaka leo ni Wamarekani weusi.
Jeb Bush ambaye ni Mgombea Urais wa Marekani ameahirisha kufanya Kampeni zake Charleston baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la kihistoria mjini Carolina Kusini amekamatwa.
Kulingana
na mwanasheria mkuu Lorreta Lynch,awali maafisa walimtaja kijana huyo
wa miaka 21 kuwa Dylann Storm kama mtu waliyekuwa wakimsaka kwa
shambulizi la Charleston.Maafisa wa polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo aliyejihami na bunduki aliketi katika mkutano wa mafundisho ya biblia kwa takriban saa moja kabla ya kufyatua risasi na kuwaua wanawake sita na wanaume watatu akiwemo mchungaji wa kanisa hilo.
Maafisa wamelitaja shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki.
Bi Lynch amesema idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini njia mwafaka ya kumfungulia mashtaka mshukiwa.
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema kuwa bwana Storm alikamatwa huko Selby Carolina kaskazini saa 13 baada ya shambulizi.
No comments:
Post a Comment