Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema anaamini
kuwa muigizaji huyo anaweza kuwa kiongozi mzuri japo changamoto
inayomkabili ni kubadilisha mawazo ya watu juu yake hasa kutokana na
maisha yake ya ustaa na mapenzi.
Martin ameiambia Bongo5 kuwa kinachotakiwa sasa ni kuwabadili watu waanze kumchukulia kama mwanamke anayeweza kuwa kiongozi.
“Watu wengi wametokea kumsupport kwa sababu walikuwa wanamsikia baba
yake akimtaka aingie kwenye siasa, na wengine walikuwa wanamtaka Wema
aingie kwenye siasa,”amesema Martin.
“Lakini ana kazi kubwa ya kuweza kubadilisha watu jinsi
wanavyomchukulia. Kwahiyo anachukulia positive kwa sababu watu aliokuwa
nao wameweza kumsupport. Lakini kabla hatujafika huko sasa tutamuona
kama kiongozi sioo kama msichana wa bongo movie. Tumuamini Wema kama
anaweza kuonyesha tu nia hata asipopata tukumbuke kuonyesha nia tu ni
kupata, kwa sababu ana ndoto kubwa sana anataka kuzifanya,” ameongeza.
Hivi karibuni Wema alitangaza nia ya kuwania ubunge wa viti maalum kwa tiketi cha chama cha mapinduzi mkoani Singida.
No comments:
Post a Comment