Wananchi wa kijiji cha kimbushikata ya machame wilayani hai mkoani kilimanjaro wamelalamikia hatua ya diwani wa kata hiyo kuzuia misaada inayotolewa na viongozi wa vyama vya upinzani isitumike katika kata yake ukiwemo wa matengenezo ya barabara uliotolewa na mwenyekiti wa taifa wa chadema freeman mbowe.
ITV imetembelea kata hiyo na kuzungumza na wananchi ambao pamoja na kumsukuru Mh.Mbowe kwa msaada huo wa Greda la kutengeneza barabara wamelaani vikali kitendo cha diwani huyona wameiomba serikali kutofumbia macho vitendo vya aina hiyo.
Akizungumzia malalamiko hayo mwenyekiti wa taifa wa chadema Mh.Freeman Mbowe ambaye pia ametembelea kata hiyo amewataka wananchi kutokubali kugawanywa kwa itikadi za kisiasa kwani lengo la siasa ni kuleta maendeleo na wala sio kukwamisha maendeleo.
Hatua hiyo pia imekemewa na waziri wa ujenzi Mh.John Magufuli na mkuu wa mkoa wa kilimanjaro waliokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya barabara katika mkoa wa huo.
No comments:
Post a Comment