Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limetoa onyo kali kwa askari wa polisi jamii kuacha tabia ya kutumia kivuri cha jeshi ilo kutenda maovu kwa kuonea raia na pengine kunyang’anya mali za watu kwakuwa lengo la kuanzishwa kwake ni kusaidia jamii na siyo kuikandamiza.
Kwa upande wao vijana hao wanashiriki katika ulinzi shirikishi wamesema wanakabiliwa na hali ngumu ya vitendea kazi kama usafiri na kwamba wanapokuwa katika ulinzi nyakati za usiku wanakutana na matisho mengi kutoka kwa waharifu wenye silaa kali wamelitaka jeshi ilo kuongeza idadi ya askari wanaoshirikiana nawo pamoja na silaa.
Diwani wa kata ya moshono Paulo Mattysen amesema kwa kushirikia na viongozi wa pilisi hakuna kitakacho haribika kwani anaimani kuwa mapungufu yatafanyiwa kazi kuimalisha ulinzi shirikishi kwakuwa eneo ilo linamatendo mengi ya uharifu hivyo polisi jamii wana nafasi kubwa.
No comments:
Post a Comment