TTCL

EQUITY

Wednesday, March 4, 2015

Waasi waviteka visima vya mafuta Libya

Visima vya mafuta nchini Libya.

Wapiganaji wa kiislamu wameripotiwa kuviteka visima viwili vya mafuta katikati mwa Libya huku makundi hasimu yakiendelea kupigania udhibiti wa taifa hilo.
Vikosi vinavyolinda visima vya mafuta vya al Bahi na al Mabruk vilisalimu amri baada ya kuishiwa na silaha.
Serikali ya Libya inayotambulika kimataifa mjini Tobruk inakabiliana na mahasimu wake wa Libya Dawn ambao wanadhibiti mji mkuu wa Tripoli.
Pande hizo mbili pia zilishambuliana siku ya jumanne.
''Watu wenye itikadi kali walichukuwa udhibiti wa maeneo ya al Bahi na al Mabruk na sasa wanaelekea kudhibiti kisima cha mafuta cha Al Dahra kufuatia kusalimu amri kwa vikosi vilivyokuwa vikilinda maeneo hayo'',alisema kanali al_Hassi, msemaji wa usalama wa sekta ya mafuta.

No comments:

Post a Comment