- Mwako 2014 ukiwa unaendea ukingoni kumalizika, waigizaji Jackline Wolper na Kajala Masanja pamoja nawaigizaji wengine akiwemo Hemmedy Selemani " Hemmedy PHD" wameonekana wapo mzigoni kutengeneza filamu mpya.
Akiweka picha hii mtandaoni leo asubuhi, Wolper alii-caption;
“Watu wengne tumenuna kuamshwa mapema wengne wanatabasam..jamani haya bana ..new movie location day2 Mungu tusimamie”
Akionyesha kuwa wapo kambini, na badae Kajala kuongeza kwa maneno “@tegeta location moja....." akimaanisha kuwa wapo maeneo ya Tegeta hapa Jijini Dar-es-salaam.
Jana usiku kwa nyakati tofauti Kajala na wolper walitupia picha mbalimbali mtandaoni huku “captions” zao zikisomeka kuwa wapo kazini hadi muda huo, kama baadhi ya picha unavyoziona hapo juu.
Ingawa bado hawajaweka wazi jina la filamu hii na kusema itatoka lini,wapenzi na mashabiki wengi wameonyesha shauku kubwa ya kuona kazi hiyo na hivyo wanaisubiri kwa hamu kwani wengi wanadai hili- “Collabo”sio la mchezo kwahiyo wanategemea kazi nzuri na bora zaidi.
No comments:
Post a Comment