TTCL

EQUITY

Tuesday, October 28, 2014

Wizi wa magari yasio na ufunguo wazidi

Range Rover
Magenge ya uhalifu yanaendelea kuyalenga magari yasio na funguo.
Kulingana na kundi moja la kampuni za magari nchini Uingereza,wezi hao huweza kulemaza mfumo wa usalama wa magari hayo kupitia vifaa vinavyotumika na fundi wa magari.
Hatahivyo watengezaji hao wa magari wanajaribu kuwa mbele ya teknolojia inayotimiwa na wezi hao kwa kuimarisha programmu inayotumika.
Imeripotiwa kuwa wamiliki kadhaa wa magari ya Range Rover nchini Uingereza wamenyimwa bima kutokana na swala hilo.
Na huku umaarufu wa magari yasio na funguo ukiongezeka,wezi wamekuwa wakinunua vifaa kupitia njia ya mitandao ambavyo vinaweza kuyafungua magari hayo.
''Uhalifu wa kuiba magari kupitia utengezaji wa rimoti zinazotumika kama funguo ni tatizo kubwa'', ilisema kampuni ya Jaguar Land Rover.
''Hatahivyo tunalichukulia swala hilo na uzito mkubwa huku timu yetu ya wahandisi wakiendelea kufanya kazi na kampuni za bima na maafisa wa polisi ili kutatua swala hili''..

No comments:

Post a Comment