Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu.
Sakata
la Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri, limeingia
katika sura mpya baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kueleza kuwa
linasubiri uchunguzi ukamilike na litamvua taji hilo endapo itabainika
kweli alichakachua umri wake.
Kufuatia ushindi alioupata siku ya shindano la kumsaka Miss Tanzania 2014 lililofanyika Oktoba 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, kuliibuka madai kwamba mrembo huyo alidanganya umri.
MADAI YA JUKWAANI
Awali, akiwa jukwaani kujitambulisha na kujibu maswali, mlimbwende huyo alishika kipaza sauti na kusema:
“My name is Sitti Mtemvu, ‘am eighteen years old (jina langu ni Sitti Mtemvu, nina miaka kumi na nane).
LUNDENGA ATOA TAMKO, ATETEA
Kufuatia hali ya
hewa kuchafuka kwenye mitandao, redio na magazeti akishutumiwa Sitti,
Oktoba 21, mwaka huu, mratibu wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim
Lundenga aliitisha mkutano na vyombo vya habari.
Cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
Katika mkutano huo ambao Sitti naye alishiriki sanjari na mama yake
mzazi, Lundenga alisema vyeti vya kuzaliwa alivyowasilisha mshiriki huyo
kama washiriki wengine, vilionesha ana miaka 23, alizaliwa 1991, Temeke
jijini Dar.
UTATA WAIBUKA
Utata ulianza kuibukia hapo kwenye maneno ya kutoka kwenye kinywa cha Lundenga kwani alisema cheti hicho kilitolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) Septemba, mwaka huu ikiwa ni siku 32 tu kabla ya shindano la Mlimani City.
Utata ulianza kuibukia hapo kwenye maneno ya kutoka kwenye kinywa cha Lundenga kwani alisema cheti hicho kilitolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) Septemba, mwaka huu ikiwa ni siku 32 tu kabla ya shindano la Mlimani City.
MASWALI
Waandishi walitaka
kujua hivi; kama cheti hicho kilitolewa Septemba 9, mwaka huu na Sitti
amesoma Marekani ambako mtu huwezi kwenda mpaka uwe na paspoti na ili
upate paspoti lazima uwe na cheti cha kuzaliwa je, yeye alitumia cheti
gani? Maana alikwenda Marekani kati ya mwaka 2010 na 2011.
Leseni ya udereva ya miss Tanzania Siti Mtemvu.
vyombo vya habari vinamfuatafuata sana.
UFUKUNYUKU WAANZA
Kufuatia mlolongo huo wote,
ndipo timu ya uchunguzi ya Magazeti Pendwa ya Global Publishers ikaingia
mtaani na kuanza kuchimba ukweli wa umri wa binti huyo.
Katika
chanzo cha uhakika kutoka katika idara husika ya kutoa paspoti, faili la
Sitti lilisomeka hivi: (tunaandika kwa Kiswahili tu).
Pasipoti ya miss Tanzania Siti Mtemvu.
SHULE ALIYOSOMA UGANDA
Ufukunyuku wa gazeti hili
ulikwenda mbele zaidi hadi kwenye Shule ya Sekondari ya Hana Mixed
iliyopo Mji wa Nsangi, Kampala, Uganda ambako Sitti alisoma kidato cha
tano na sita.
Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la jina lake
kutoandikwa gazetini, mwanafunzi mmoja alisema kuwa, mwaka 2006 Sitti
aliingia shuleni hapo kidato cha tano akiwa na miaka 17. (Piga hesabu
mpaka mwaka huu).
BETHIDEI YAKE 2007
Mwanafunzi huyo akazidi kudai
kuwa, Mei 31, 2007, Sitti akiwa kidato cha sita, alifanya sherehe fupi
ya kuadhimisha kuzaliwa kwake ‘bethidei’ ambapo alisema anatimiza mwaka
wa 18.
Sitti Abbas Zubeir Mtemvu.
Katika kasherehe hako ambako hakakuwa rasmi, waliohudhuria ni kijana
mmoja na wanafunzi waliokuwa wakilala chumba kimoja na Sitti. Sitti
alimaliza kidato cha sita Novemba 2007.
MNYAMBULISHO WAKE
Kwa hesabu za haraka, Sitti
alianza darasa la kwanza akiwa na miaka 6 (1995). Darasa la 7 akamaliza
akiwa na miaka 12 (2001). Alianza kidato cha kwanza akiwa na miaka 13
(2002), akamaliza kidato cha 4 akiwa na miaka 16 (2005). Akiwa na miaka
17 alianza kidato cha 5 (2006), akamaliza cha 6 akiwa na miaka 18
(2007).
No comments:
Post a Comment