TTCL

EQUITY

Saturday, October 25, 2014

MAHAKAMA YAMPA CHRIS BROWN ADHABU NYINGINE {2014}



Chris Brown ataendelea kusota na adhabu za jela japo kwa kazi za nje. Kwa mujibu wa TMZ, hitmaker huyo wa Loyal aliyependa kizimbani jana kusikiliza maendeleo ya msala wake, atakuwa busy hadi Januari 2015 kutumikia kazi za jamii. 

 Chris Brown amepewa ‘adhabu’ ya kufanya kazi za kijamii kwa masaa nane kila siku, na kwa mujibu wa ratiba aliyopewa na mahakama anatakiwa afanye kazi hizo kwa siku 4 kila wiki, ikiwa ni siku 1 tu ndani ya wiki kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa ambazo atakuwa na mambo yake mengine. 

Daktari wake alijaribu kupeleka utetezi wake kwa Chris ili kumnusuru na adhabu hiyo hiyo kutokana na matukio kadhaa aliyoyafanya kipindi akiwa chini ya uangalizi wa mahakama juu ya mwenendo wake baada ya kukabiliwa na kesi ya kumpiga mpenzi wake wa zamani, Rihanna

No comments:

Post a Comment