Antoine Christophe Mumba “Koffi Olomide’’
Mzaliwa wa Jamhuri ya Watu wa Kongo, alizaliwa mwaka 1956, ni mmoja wa
wanamuziki wa zamani ambao hawajawahi kuchuja tangu aanze muziki.
Youssou N’dour:
Mkongwe toka Senegal, aliyezaliwa mwaka 1959, ndiye tajiri kwa
wanamuziki wa Afrika, akimiliki chombo cha habari kikubwa nchini mwake,
ni mwimbaji, mtunzi mwigizaji, mfanyabiashara na mwanasiasa, aliwahi pia
kuwa Waziri wa Utamaduni na Maliasili nchini Senegal.
P.Square:
Peter na Paul Okoye toka Nigeria, wanashika nafasi ya pili kwa utajiri,
barani Afrika kwa zaidi ya dola 150,000/= kwa shoo. Kwa sasa wanafanya
kazi na lebo ya Akon ‘’Konvict muziki’’ na pia walishafanya kazi na
Kampuni ya Universal Music South Africa.
Dapo Daniel Oyebanjo
‘’D’banj’’ alizaliwa nchini Nigeria mwaka 1980, ni mwanamuziki na
mjasiriamali, ameshawahi kuchukua tuzo kadhaa zikiwemo za MTV, BET na
nyinginezo.
Salif Keita:
Alizaliwa mwaka 1949, ni mmoja wa wasanii matajiri Afrika mwenye ulemavu
wa ngozi (Albino) ana sauti nzuri na anamiliki bendi yake, kisiwa na
kiwanja kikubwa nchini Ufaransa.
Fally Ipupa Nsimba:
Mwanamuziki toka Jamhuri ya Watu wa Kongo, alizaliwa mwaka 1977, aliwahi
kuwa katika bendi ya Koffi Olomide, ni mwimbaji, mtunzi, mpiga gitaa,
anayesifika kwa kukata mauno awapo jukwaani, amewahi kushinda tuzo
kadhaa za MTV, Kora na nyinginezo.
Innocent Ujah Idibia
‘’2face Idibia’’ alizaliwa Jimbo la Jos nchini Nigeria, ni mtunzi,
mwimbaji na mtayarishaji wa muziki, amewahi kushinda tuzo kadhaa
zikiwemo za MTV, Channel O, BET, Kora na MOBO.
No comments:
Post a Comment