TTCL

EQUITY

Monday, September 1, 2014

Watanzania washauriwa kuwekeza kwa kuwajali watoto

Mkuu wa Kitengo cha Usuluishi na Ushauri wa Sheria (katikati) akisisitiza jambo kwa wanahabari alipokuwa akitoa tamko kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Valerie Msoka. Kushoto ni Mwanasheria wa Tamwa, Loyce Gondwe na kulia ni Mwanachama wa TAMWA, Marie Shaba. Mkuu wa Kitengo cha Usuluishi na Ushauri wa Sheria (katikati) akisisitiza jambo kwa wanahabari alipokuwa akitoa tamko kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Valerie Msoka. Kushoto ni Mwanasheria wa Tamwa, Loyce Gondwe na kulia ni Mwanachama wa TAMWA, Marie Shaba.
 
Mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wawakilishi wa TAMWA wakisoma tamko lao juu ya umuhimu wa jamii kuwajali watoto. Mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wawakilishi wa TAMWA wakisoma tamko lao juu ya umuhimu wa jamii kuwajali watoto.
 
 Mwanachama wa TAMWA, Marie Shaba (wa kwanza kulia) akizungumza katika semina kwa baadhi ya wanahabari juu ya uandishi wa habari za kuwatetea watoto.   Mwanachama wa TAMWA, Marie Shaba (wa kwanza kulia) akizungumza katika semina kwa baadhi ya wanahabari juu ya uandishi wa habari za kuwatetea watoto. 

  CHAMA cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA) kimeitaka Serikali na jamii kwa ujumla kuwekeza katika kumuandaa mtoto kwani licha ya kuwa zawadi kubwa, watoto pia ni tumaini na uhai wa taifa kuendelea. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka katika taarifa iliyosomwa kwa wanahabari jijini Dar es Salaam kuhamasisha jamii kwa ujumla kuwajali watoto hasa kwenye mchakato unaoendelea hivi sasa wa uundaji wa Katiba Mpya. TAMWA ilisema mabadiliko ya sera za siasa na uchumi kwa kiasi kikubwa yameathiri
namna taasisi za kijadi na kidini zinavyofanya kazi na kujikuta zikijiondoa kwa namna moja ama nyingine katika suala zima la kuwasaidia pamoja na kuwalinda watoto. "...Leo hii mzigo mkubwa wa malezi umeachiwa Serikali kwa kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na ile ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Ajira na Kazi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, taasisi za kidini, asasi zisizo za Kiserikali, Televisheni, sinema, wasanii na hata majambazi nao wanalea watoto," ilisema taarifa hiyo. Alisema kwa sasa Wizara nyingi zinaamini hazihusiki na watoto hivyo kujikuta sera na sheria zao nyingi kuwasahau watoto. Alisema suala la watoto ni mtambuka hivyo kula kila sababu ya kufanya mabadiliko yoyote ya sera na sheria kuwa na manufaa zaidi kwa watoto hasa katika kipindi hichi cha mabadiliko ya katiba. Aliongeza kuwa suala la malezi ya mtoto ni jukumu la kila mmoja na sio kuwaachia baadhi ya watu tena wawalee watoto hao wanavyojua wao kwa maslahi yao pekee. Watoto ni zawadi kubwa na tumaini la taifa kuendelea hivyo kuna kila sababu ya kuwekeza katika kundi hilo. "...Tujipange ili tusiendelee kudharauliwa kuwa hatuna uwezo wa kuwapenda na kuwalea kwa ajili ya ufukara. Ni dhabi kusikia kuwa umemchoma moto mtoto kwa kuiba shilingi mia kwa ufukara. Au wengine kunajisi watoto wadogo kwa kisingizio kuwa ufukara ndio umekusababisha utende hayo. Tunasema huo ni zaidi ya unyama...tuache kuvumilia aina yoyote ya ukatili unaowafanya watoto wakose furaha, upendo na matumaini," alisema katika taarifa yake. Mkurugenzi huyo wa TAMWA alisema zamani enzi za bibi na babu taasisi za jamii zilisaidia kumtayarisha kijana juu ya nmna ya kuishi na watu, majirani, wenzi wake huku suala la malezi ya watoto likiwa ni jukumu la jamii nzima jambo ambalo kwa sasa limekoma baada ya kuingia utandawazi. Alibainisha kuwa kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza katika dhana nzima ya malizi kwa watoto hatuwezi kurudia kama ilivyokuwa enzi za mabibi na mababu bali inaweza kutumika falsafa zao na kujikuta tunaendelea kuendesha maisha yetu kwa sasa. Alisema ipo haja ya kuchambua jinsi gani shule na hata malezi ya nje ya shule yanavyoweza kuwa pahala pa kunoa na kumpiga msasa mtoto ili afikie umri wa miaka 18 awe amehitimu, anaheshimu haki zake na za wengine, aweze pia kuishi kwa kujitegemea na kutumia elimu na ujuzi alioupata kwa faida ya jamii. Hata hivyo aliitaka jamii kuunga mkono juhudi zote chanya zinazowekwa ili kujenga mazingira mazuri ya kumfanya mtoto aweze kuishi kwa amani, furaha, upendo na matumaini.

No comments:

Post a Comment