TTCL

EQUITY

Sunday, May 4, 2014

TZ Celebrity || DIAMOND ANYAKUWA TUZO ZOTE KILL MUSIC FID Q KATOKA NA ZAKE{2014}

Diamond Platnumz ndiye msanii namba moja kwa sasa nchini Tanzania baada ya usiku wa Jumamosi kunyakua vipengele vyote zote saba alivyokuwa ametajwa kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro, KTMA.



  Muimbaji huyo aliyekuwa ameambatana na mchumba wake Wema Sepetu amechukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka, wimbo bora wa afro pop na video bora ya mwaka kwa wimbo wake ‘My Number On’e pamoja na Muimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya, Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki na Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya.
 Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kulia) akimkabidhi tuzo Diamond, kushoto ni producer wa My Number One, Sheddy Clever Wema akimkumbatia Diamond
 Msanii mwingine aliyeshangaliwa zaidi katika usiku wa tuzo hizo ni Fid Q aliyenyakua tuzo mbili ambazo ni Msanii Bora wa Hip Hop na Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop.

   Na kundi la Weusi limeibuka na tuzo mbili, Wimbo bora wa Hip Hop (Nje ya Box – Nick wa Pili ft Joh Makini & G-Nako) na kundi bora la mwaka la kizazi kipya.



                  Chini hapo Vanessa Mdee akimbusu Lulu baada ya kukabidhiwa tuzo ya wimbo bora wa R&B

       Mzee wa  badilisha Jose Chameleone akipokea tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki


        Isha Ramadhan akipokea tuzo   Wasanii waliotumbuiza


                              Wasanii wa Kenya, Amani na Wyre wakimkabidhi tuzo Luiza Mbutu
Usiku Wa ulipambwa na wasanii    Mwana FA, Weusi, Madee, Vanessa Mdee, Meninah, Angel, Makomando, Msami, Twanga Pepeta, Extra Bongo na wengine.
Orodha nzima Ya Washindi Wa Zuzo hUsiku wa kill. Wimbo bora wa mwaka Number One – Diamond
 Mwimbaji bora wa kike – kizazi kipya Lady Jaydee  M
uimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya Diamond
Muimbaji bora wa kike taarab Isha Ramadhan
Muimbaji Bora wa kiume – Taarab Mzee Yusuf
Muimbaji bora wa kiume – Bendi Jose Mara
Muimbaji Bora wa Kike – bendi Luiza Mbutu
 Msanii Bora wa Hip Hop Fid Q
  Msanii Bora Chipukizi Anayechipukia Young Killer
 Rapa Bora wa Mwaka – Bendi Furguson
Mtumbuizaji bora wa kike muziki Isha Ramadhani
Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki Diamond
Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop Fid Q
Video Bora ya Mwaka Number One – Diamond
 Bendi ya Mwaka Mashujaa Band
Kikundi cha Mwaka cha Taarab Jahazi Modern Taarab
 Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya Weusi
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Taarab Enrico
  Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Kizazi kipya Man Walter
 Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Bendi Amoroso
 Mtunzi Bora wa Mwaka – Taarab Mzee Yusuf
 Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya Diamond
  Mtunzi Bora wa Mwaka – Bendi Christian Bella
Wimbo bora wa Kiswahili – Bendi Ushamba Mzigo – Mashujaa Band
 Wimbo bora wa reggae Niwe na Wewe – Dabo
Wimbo bora wa Afrika Mashariki Tubonge – Jose Chameleone
 Wimbo bora wa Afro Pop Number One – Diamond
 Wimbo bora wa Taarab Wasiwasi Wako – Mzee Yusuf
 Wimbo bora wa Hip Hop Nje ya Box – Nick wa Pili f/ Joh Makini & G-Nako
Wimbo Bora wa R&B Closer – Vanessa Mdee
 Wimbo Bora wa Kushirikiana Muziki Gani – Nay wa Mitego ft Diamond
Wimbo bora wa ragga/dancehall Nishai – Chibwa f/ Juru
Wimbo bora wa zouk /rhumba Yahaya – Lady Jaydee
Hall of FAME Award Hassan Rehani Bichuka
 Masoud Masoud – TBC Taifa

No comments:

Post a Comment