Vicky Paschal Kamata.
“Kuna mizengwe mingi sana kwenye hii ndoa japokuwa iko katika hatua za mwisho lakini hatihati. Wapo watu wanasema kuwa mwanaume anadaiwa ana mwanamke mwingine, wengine wanasema ana mchumba ameshamlipia maharikwa wazazi wake kwa hiyo mambo yameshajulikana na jamaa akaona aachane na ndoa hiyo.
“Lakini katika yote hayo, ukweli ni kwamba kuna asilimia tisini ya ndoa kutofungwa hiyo Mei 24 ndicho ninachokijua mimi,” alisema mtu mmoja wa karibu na familia ya wachumba hao.
Vicky alipotafutwa kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Hata hivyo, Uwazi bado linayafanyia kazi madai hayo ambayo ni mazito na ya ndani.