HIZI NDIZO SABABU ZA WANAWAKE KUTEMBEA NUSU UCHI
Kuna
wakati wanaume hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa
wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana
kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa
fidia kutokana na kuamini kwao kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo
miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.
Wakati
mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa
wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa
fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa
zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba,
pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.
Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au
kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo
kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri.
Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani,
kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.
No comments:
Post a Comment