Ngassa akiwa kimahaba na Snura.
Na Hamida Hassan
Staa wa sinema na muziki Bongo, Snura Anton Mushi na Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa wamenaswa ‘laivu’ wakiwa kimahaba, Amani lina mkanda kamili.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, tukio hilo lililijiri hivi karibuni nyumbani kwa Snura maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambapo wawili hao walibambwa wakiwa wamejiachia ‘wakifanya yao’.
Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na majirani zake.
Ngassa akimbusu Snura.
“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
“Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.
Ili kujiridhisha, Amani lilisaka picha za wawili hao ambazo walikuwa ‘wakijifotoa’ kwa simu zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo lililozua utata na maswali kwa walioziona.
...Wakiwa katika pozi.
Baada ya kulishwa ‘niuzi’ hizo, gazeti hili lilimsaka Snura ambapo alipopatikana alitakiwa alimwagiwa habari yote juu ya uhusiano wake tata na Ngassa ambapo alikuwa na haya ya kusema:
...Ngassa akimsuka Snura.
“Ngassa alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu. Simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo.”
...Wakizidi kujiachia kimahaba.
No comments:
Post a Comment