urundika taka taka kihorela katika mitaa yetu |
Mazingira ni
vitu vyote vile vinavyotuzunguka katika maisha tunaoishi ama maeneo tunayoishi. Mazingira yanaweza
kumfanya mtu kuwa katika afya iliyobora na isiyo bora kuwa na afya bora,
pamoja na kuendelea kuwa na afya bora ni wajibu wa kila binadamu.Tunahitaji
kuwa na miili yenye afya bora na nguvu ili tuweze kuendelea na shughuli zetu za
kila siku katika ujenzi wa wa Taifa. Kila binadamu ana marengo aliyojiwekea
katika maisha na ili marengo hayo yatimie ni lazima mwanadamu huyo awe na afya
iliyo bora zaidi. Ni wazi kabisa katika nyakati hizi, na katika jamii
tunayoishi, kiwango cha usafi wa mazingira ni duni sana na hamna viwango maalum
vilivyowekwa katika kuyaweka mazingira safi.
Nadhani kitu kikubwa
kinachotufanya tuwe hivi na kutojali kuyaweka mazingira yetu yawe safi, ni
mazoea tuliyokuwa nayo na tumekulia katika mazingira yasiyo safi hali
iliyotufanya tuzoee mazingira yasiyo safi. Tazama vyakula vinavyouzwa mtaani bila
kufunikwa katika vumbi jingi na moshi mzito utukanao na magari na shughuli
nyingine, lakini tunanunua na kula. Ni ukweli kuwa ulaji huo hupelekea
kupata magonjwa ambayo hutufanya tujikute katika hospitali mbali mbali
tukihangaika kuokoa maisha yetu. Ni gharama kwetu na gharama kwa Taifa kwa
ujumla.
Tazama wasafiri wa
vyombo mbalimbali vya majini, mijini, katika mikoa na hata nje ya nchi
watupavyo taka katika mazingira bila kujali uharibifu, bila kujali kama ni
mbuga ya wanyama, kama ni chanzo cha maji na hata bila kujali kama ni
msitu wa hifadhi.
Kama hatutatupa takataka au kuziharibu
katika njia iliyo sahihi, tutapata magonjwa mbalimbali hatari yanayotokana na
utupaji ovyo huo. Tunaweza kugawanya aina ya taka katika makundi makuu matatu.
1)
Taka za kawaida za nyumbani, ambazo nazo zimegawanyika katika taka
ngumu(plastiki,glasi, bati,mbao nk) taka laini za jikoni(mabaki ya
chakula), na maji taka(kutoka katika vyoo na mabafu).
2) Taka za viwandani kama maji taka na kemikali mbalimbali pia taka ngumu.
3) Taka za Hospitali ambazo nazo zinahitaji uangalizi mkubwa kuepuka kusambaa kwa magonjwa mbalimbali.
Taka zinazoharibu vyambo vya maji |
Asilimia kubwa ya watu
hawana mazoea ya kutupa na kuhifadhi takataka katika njia iliyo sahihi na
salama, ni kawaida kukuta taka za majumbani na hata viwandani zikiwa zimezagaa
ovyo kwenye mitaa, barabarani, majengo ambayo hayatumiki, katika mitaro,
mtoni,chini ya madaraja. Pia kwenye vyanzo mbali mbali vya maji kama bahari,
mito na maziwa na ikiwa maeneo haya ndiyo watu wengi hutumia maji haya kwa
matumizi ya nyumbani na hata kunywa. Uwepo wa taka hizi umelekea kuwepokwa
harufu mbaya na kali zaidi mpaka imekuwa kero kubwa kwa mtu kuishi kutokana na
kuepo kwa mrundikano wa taka ambazo
zinawaathiri kiafya wakazi wa maeneo hayo.
Taka zinazozalishwa na
familia zaweza kuwa hatari zisipotupwa na kuharibiwa katika njia iliyosahihi.
Taka hizi zaweza kupelekea milipuko ya magonjwa hatari, na zinapoachwa wazi
zinaweza kuchafua mazingira, na kusambaza magonjwa kupitia upepo unaovuma, wadudu
kama inzi na mende, na pia uambukizo wa magonjwa waweza kusambazwa kupitia njia
ya upumuaji. Vimelea vya magonjwa vyaweza pia kuingia katika vinywaji
visivyofunikwa, vyakula vilivyoachwa wazi barabarani na kusababisha magonjwa
kama kuhara damu, kipindupindu, homa ya tumbo, minyoo, kichefuchefu na
kutapika.
Kutunza mazingira na yakawa safi ni jukumu la kila mtu bari si la serikari pekee kwasababu kila mtu anahitaji awe na afya bora na kuwa na ili uwe na afya bora ni lazima mazingira yanayokuzunguka yawe safi. Kwa hiyo basi, kuyaweka mazingira yetu katika hali ya usafi, kutatuepusha na matatizo mengi yakiwemo magonjwa mbali mbali ya mlipuko.
No comments:
Post a Comment