TTCL

EQUITY

Friday, January 29, 2016

Tume ya haki za binadamu yanena kuhusu bunge la 11

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inafanyia uchambuzi taarifa ya serikali kupunguza muda wa matangazo ya bunge ya moja kwa moja ili kuona kama uamuzi huo hautaingilia haki ya wananchi kupata habari chini ya Ibara ya 18(d) ya Katiba

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inafanyia uchambuzi taarifa ya serikali kupunguza muda wa matangazo ya bunge ya moja kwa moja ili kuona kama uamuzi huo hautaingilia haki ya wananchi kupata habari chini ya Ibara ya 18(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Aidha, taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Bahame Tom Nyanduga imesikitishwa na vurugu zilizotokea Bungeni baada ya uamuzi huo kutolewa ambapo zilisababisha askari wa kutuliza ghasia (FFU) kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge.

Bw. Nyandugu amesema tume Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaamini kwamba vurugu siyo njia sahihi ya kupata muafaka wa mambo ambayo waheshimiwa wabunge hawakubaliani nayo.

Pia, tume imetamka kwamba kitendo cha askari wa kikosi cha FFU kuingia bungeni kuwatoa wabunge waliokuwa wakifanya vurugu ni kitendo kilichodhalilisha Bunge kama muhimili muhimu wa taifa na ni kitendo cha aibu kwa taifa.

No comments:

Post a Comment