NI shida! Zile shilingi milioni 13 alizotoa Wema Isaac Sepetu kumlipia msanii maarufu wa sinema Bongo, Kajala Masanja asitupwe gerezani, bado ni tatizo ikidaiwa kuwa sasa ngumi nje nje.
JINA LA MILIONI 13 ZA WEMA
Kwa muda mrefu sasa, Kajala amekuwa akitukanwa kwenye mitandao ya kijamii hasa matusi ambayo hayaandikiki huku akipachikwa jina la ‘Milioni 13 za Wema’ na kuahidiwa kichapo.
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Kajala, staa huyo hana raha wala furaha kwani ishu hiyo inamtesa kila kukicha.
Ilidaiwa kwamba Kajala ana mtoto mkubwa aitwaye Paula aliyezaa na prodyuza wa Bongo Records, Paul Matthysse ‘P Funk’ ambaye anajua kuingia kwenye mitandao hiyo hivyo kufedheheshwa hasa anapokuta mama yake akiitwa fuska wakati yeye anamheshimu.
KUNDI LA TEAMWEMA
Ilisemekana kwamba Wema ana
kundi linalojiita TeamWema ambalo memba wake wamekuwa wakianzisha mada
mbaya kuhusu Kajala wakimhusisha na uporaji wa aliyekuwa bwana wa Wema, Clement au CK.
Ilifahamika kwamba shinikizo kubwa la kundi hilo la Wema ni kutaka Kajala arejeshe fedha hizo ndipo mambo yakae sawa.
“Anamdharau sana Madam (Wema) wakati ndiye aliyemnusuru, sasa hivi
angekuwa jela. Kama ana fedha kama anavyotamba basi arudishe milioni
kumi na tatu twende sawa,” ilisomeka sehemu ya maoni ya TeamWema kwenye
ukurasa wao wa kijamii wa Instagram.
Kuna madai kwamba kumekuwa na mtafutano kati ya kundi la Wema na lingine jipya linalodaiwa ni la Kajala.
TIMBWILI KLABU
Kwa mujibu wa shushushu wetu
ndani ya Ukumbi wa Maisha uliopo Masaki, Dar, wiki iliyopita, usiku wa
manane, wawili hao walikutana ndipo kukatokea timbwili huku jina la
Milioni 13 za Wema likiendelea kutajwa mara tu Kajala alipoonekana ukumbini hapo.
Habari zilidai kuwa wawili hao walianza kwa kushindana kumtuza Snura
Mushi aliyekuwa akifanya shoo jukwaani ndipo wapambe wao wakaingilia
kati na ‘kuinunua kesi’.
Ikadadavuliwa kuwa tukio hilo lilichochea kundi la Wema kuanza vurugu huku lile la Kajala nalo likijibu mapigo.
KAJALA NDUKI
Hata hivyo, ilisemekana kwamba
baada ya Kajala kuona hali inazidi kuwa mbaya alitumia busara kwa kutoka
nduki lakini kundi hilo la Wema lilizidi kumfuata hadi kwenye gari lake wakitaka kumdhuru.
“Kuna watu walimfuata kabisa hadi kwenye gari na wengine walikuwa
wanatafuta mawe walipopoe gari lake lakini Mungu mkubwa hawakufanikiwa,”
alisema shuhuda wetu.
BOFYA HAPA KUMSIKIA KAJALA
Baada ya kunyaka
habari hiyo, gazeti hili lilimtafuta Kajala ambaye alidai kuwa yeye
hakushuhudia tukio hilo lakini akakiri kuwa hana uhusiano mzuri na Wema.
“Mimi kwa upande wangu sina tatizo na Wema lakini natukanwa sana bila sababu. Sijui nimemfanyia nini kibaya.
“Narudia tena sina tatizo na Wema halafu siyo yeye anayenitukana au
kunisakama, ni kundi linalojiita TeamWema. Sina uhakika kama yeye ndiye
anawatuma.
“Kuhusu milioni 13, sasa nitazirudishaje wakati hakunikopesha,
alinilipia bure? Hata sijui kama nikizirudisha nitakuwa sahihi? Sielewi
lakini kama ni matusi, kweli natukanwa sana hadi mwanangu anaona
ninavyoitwa malaya,” alisema Kajala kwa uchungu.
Alipoulizwa kama yupo tayari kupatanishwa na Wema, Kajala alisema
yeye hana kipingamizi kwani yupo tayari wakati wowote ili aishi kwa
amani.
Jitihada za kumpata Wema ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.
MILIONI 13 KIVIPI?
Wema alimlipia Kajala Sh.
milioni 13 kama faini baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano
alipopatikana na hatia ya kushirikiana na mumewe Faraji Agustino Chambo
katika utakatishaji wa fedha haramu. Katika hukumu hiyo mume wa Kajala
alitupwa jela kifungo cha miaka saba.
-GPL
No comments:
Post a Comment