OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers inaendelea! Wiki hii ilifanya kazi nyingine nzito, kumnasa Pastor John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance lililopo Masaki, Dar ambaye alinaswa akichezewa utupu na wanawake watatu ambao ni kama waumini wake kwa sababu wote ni Wakristo.
Pasta
John Paul Simon Rubanguka wa kanisa la kiroho la Maximum Deliverance
lililopo Masaki, Dar baada ya kunaswa na wanawake watatu wakimchezea
utupu.
OFM YATONYWA UCHAFU WA PASTOR
Ilikuwa Jumanne ya Aprili Mosi, 2014, saa 4:14 asubuhi, chanzo cha habari kilipiga simu chumba cha habari cha Global na kuwataka makachero wa OFM ambapo alipounganishwa nao alisema:
“Jamani kama kweli hapo ni OFM nina malalamiko. Mimi nimeshtukia mchezo mchafu unaotaka kufanywa na pastor (mchungaji) mmoja anaitwa Rubanguka.
Pasta John Paul Simon Rubanguka akijaribu kujitetea.
“Huyu
pastor amempa dili dada mmoja kumtafutia wasichana wazuri watatu na
kuwapeleka kwenye nyumba moja hivi kisha wawe wanamchezea utupu wake
huku wao wakiwa kama walivyozaliwa, ndiyo furaha yake ilipo. Wasichana
wameshapatikana.”
MSHIKO WA NGUVU NA SAFARI JUUMtoa habari huyo aliendelea kudai kuwa, pastor huyo alisema wasichana watakaokuwa wakichezea utupu atawafanyia usaili wa kwenda kuwauza kwenye kasino moja iliyopo Uarabuni ambayo yeye ni wakala wa kuwapelekea malaya huko.
Pastor akiwa na mmoja wa wanawake waliofumaniwa naye.
Chanzo
hicho kiliendelea kudai kuwa, pastor huyo aliwaahidi wanawake hao
kitita cha shilingi 300,000 kila mmoja kwa wale watakaofaulu kumchezea
vizuri, sanjari na kuwakatia hati za kusafiria ‘passport’.
Makamanda wa OFM wakimtuliza Pasta.
OFM YAWEKA MTEGOBaada ya kupata ishu nzima, OFM ilifanya ukachero na kugundua mahali ambapo tukio hilo lilipangwa kufanyika, ni kwenye danguro moja lililopo Kinondoni jijini Dar.
Wanawake walionaswa katika tukio hilo wakivaa viwalo vyao.
OFM
ilifika kwenye nyumba hiyo na kufanya ushushushu wake ambapo
walifanikiwa kuweka mitambo yao sambamba na kulishirikisha jeshi la
polisi kwa ajili ya kumnasa mtumishi huyo wa Mungu akifanya vitendo
hivyo.
Saa
8:11 mchana, OFM wakiwa wamejibanza eneo hilo waliwashuhudia warembo
watatu, weupe wakielekea kwenye nyumba ambayo mtoa habari wetu
aliielekeza.
PASTOR AWASILI KWA MBWEMBWE
Saa 11:23 jioni, OFM wakiwa hawajaanza hata kujisikia kuchoka, walimwona pastor huyo akiwasili kwa mbwembwe akiwa ndani ya gari dogo na kugeuza kwa staili ya kupiga ‘norinda’ kisha akashuka. Mkononi alishika maji makubwa. Alipokelewa na mmoja wa wanawake hao.
Saa 11:23 jioni, OFM wakiwa hawajaanza hata kujisikia kuchoka, walimwona pastor huyo akiwasili kwa mbwembwe akiwa ndani ya gari dogo na kugeuza kwa staili ya kupiga ‘norinda’ kisha akashuka. Mkononi alishika maji makubwa. Alipokelewa na mmoja wa wanawake hao.
Saa 11:40 jioni, makachero wa OFM walifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa, tayari mchezo ulishaanza ambapo waliwataarifu polisi na kuungana nao kwenda kuvamia nyumba hiyo.
Msafara wa OFM na polisi hao ulifika nje ya chumba kilichokuwa kikidaiwa kufanyika uchafu huo. Sauti ya muziki na wanawake waliokuwa kama wapo kwenye darasa la siri zilisikika.
Polisi waligonga mlango na kujitambulisha kisha wakaomba wafunguliwe mlango haraka ndani ya sekunde chache.
PASTOR APATA MCHECHETO
Pasta John na wanawake hao walitii amri kwa kufungua mlango ambapo mchungaji huyo alikumbwa na mchecheto na kutaka kurukia juu ya dari lakini polisi walimtafadhalisha kutulia pamoja na wanawake hao kama walivyo.
OFM ikiwa chumbani humo iliwashuhudia wanawake hao wakiwa watupu mbele ya pastor huyo ambapo walikuwa wakimnengulia viuno.
Baada ya kupewa kibano, warembo hao walimwanika pastor huyo kwamba ndiye aliyewatuma wamchezee wakiwa watupu ili awalipe shilingi laki tatu kila mmoja, pia kuwapeleka Uarabuni kwenye kasino.
UTETEZI WA PASTOR
Kwa upande wake, Pastor John alijitetea kuwa anaomba asamehewe kwa gharama zozote ili taarifa hizo zisifike popote kwani ishu hiyo ilikuwa si amri yake bali shetani alimpitia.
“Jamani naomba tumalize humuhumu ndani, mnajua mimi ni Pastor wa Kanisa la Maximum Deliverance, sasa ukweli ni kwamba waumini wangu hawatanielewa, chondechonde ilindieni kazi yangu jamani,” alijitetea.
Mpaka OFM inaondoka eneo la tukio, pastor huyo na wanawake ‘wake’ walikuwa kwenye harakati za kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zinazostahili.
KUTOKA MEZANI KWA MHARIRI
Siku zote kazi ya OFM ni kuwajibikia matendo maovu na si kuwaonea watu kwa lengo la kuwachafua. OFM inapopata habari huichunguza ukweli wake kwanza kabla ya kuchukua hatua ya kuifanyia kazi moja kwa moja, yaani kufika kwenye eneo la tukio.
Lengo
kubwa la kutoa habari za aina hii ni kuwakumbusha watu namna ya kuishi
maisha yanayompendeza Mungu. Wengi wamebadilika, sasa wanaishi vizuri
wakiwa watu wapya na wanyenyekevu pia wenye kufundisha wenzao.
No comments:
Post a Comment