TTCL

EQUITY

Saturday, November 2, 2013

POLISI TANZANIA WAMKAMATA MFANYABIASHARA ANAYEDAIWA KUFADHILI UGAIDI

Mfanyabiashara wa Kitanzania aliyetambulika kwa jina la Juma Abdallah Kheri ambaye pia anafahamika kama Chief Abiola au Juma Sahel, alikamatwa siku ya Alhamisi, Oktoba 31, 2013 mkoani Tanga kufuatia taarifa za kijasusi zilizomuunganisha na shughuli za kufadhili vitendo vya kigaidi nchini Tanzania.

Kheri anatuhumiwa kufanya kazi na kukifadhili Kituo cha Vijana wa Kiislamu (MYC), tawi la al-Shabaab nchini Kenya.
"Anashikiliwa mikononi mwa polisi pamoja na watu wengine wawili na mahojiano yanaendelea. Kwa hivyo, siwezi kusema zaidi ya hapo sasa," kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, amekaririwa akiiambia Sabahi.

Massawe alisema mkoa wa Tanga unaweza kuwa na al-Shabaab kutokana na ukaribu wake na Mombasa, ngome ya MYC.

No comments:

Post a Comment