KIUNGO
Mesut Ozil amekuwa akiteka vichwa vya habari tangu atue Arsenal kwa dau
la Pauni Milioni 42.5 kutoka Real Madrid, lakini anaonekana kuekwa
akili mno na mpenzi wake, mlimbwende Mandy Capristo.
Nyota
huyo wa Ujerumani aliyeisaidia Arsenal kurejesha makali yake katika
Ligi Kuu England tangu atue Emirates msimu huu, alipigwa picha akimpiga
picha nyota huyo sa Pop mjini London.
Capristo,
mwenye umri wa miaka 23, ni bonge la supa staa nchini kwao Ujerumani na
kwa sasa ni msanii wa kujitegemea baada ya kujitoa katika bendi ya
wasichana wenzake, Monrose, lakini Ozil hawezi kuimba mbele ya watu.
Sema chizzz! Capristo akipozi kupigwa picha na Ozil ambaye alionekana kufurahia kufanya barabarani Jijni London
Mara tu baada ya kuwasili, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliweza kuzoeana haraka na wachezaji wenzake.
Ozil alilazimishwa kusimama kwenye kiti mbele ya wachezaji wenzake kuimba, lakini hakufurahishwa sana na hilo.
Alisema:
"Sitaki kufanya hivi tena. Sauti yangu si ya kuimba. MimiI si mshiriki
wa X Factor kwa na,na yoyote. Ulikuwa ni wimbo wa Kituruki,
kitu fulani binafsi niliimba kwa wachezaji wenzangu na ninataka ibaki
hivyo. Kwa sababu watu hawakuelewa nilikuwa ninaimba nini, lakini
walinishgilia ile mbaya, ambayo nafikiri ni babu kuibwa.
Unywele wa kimwana: Ozil na Capristo wakirejea ndani baada ya kumaliza kupigana picha
Arsenal
inamenyana na Liverpool Jumamosi hii ambayo ikiwa na kikosi chake
kamili wakiwemo wapachika mabao hatari, Daniel Sturridge na Luis Suarez
wamewasili Emirates.
Lakini
mshambuliaji Olivier Giroud amewashukuru Ozil na wachezaji wengine
wanaomtengenezea nafasi za kufunga hadi mchezaji wa nne kwa kufunga
mabao mengi katika ligi msimu huu hadi sasa.
Risasi ya Bunduki: Ozil - akiwa mazoezini Ijumaa (kulia) ametua na moto kutoka Hispania
Mastaa wapendanao: Capristo ni maarufu Ujerumani baada kung'ara na bendi ya wasichana kabla ya kuamua kuwa msanii wa kujitegemea
No comments:
Post a Comment