‘White House’ yataja sifa za Obama kuja nchini
Nairobi, Kenya. Ukitaka kumfahamu mtu, tazama
aina ya watu wanaomzunguka. Msemo huu unaweza kutumika kuielezea
Tanzania hasa baada ya kupata fursa ya kutembelewa na marais wawili wa
taifa lenye nguvu zaidi duniani.
Mara ya kwanza, Tanzania ilitembelewa na Rais wa Marekani aliyekuwapo madarakani, Bill Clinton, Agosti 28 hadi 29, 2000.
Pia, nchi ikapata tena fursa ya kutembelewa na
Rais George Bush mwanzoni mwa 2008 na sasa nchi imepata fursa tena ya
kutembelewa na rais mwingine wa nchi hiyo, Barack Obama, ambaye atakuwa
ameambatana tena na Bush, jambo ambalo ni la kihistoria kwa bara hili.
Licha ya kuwapo hali ya kutoridhika na hali halisi
ya nchi, kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoka kwa baadhi ya Watanzania,
hali inaonekana tofauti kwa Marekani ambayo mtazamo wake wa masuala ya
nchi za nje unawakilisha mtazamo wa mataifa mengi ya magharibi.
Akizungumzia sababu za ziara hiyo kwa njia ya
Conference call kutoka Washington, Makamu wa Ushauri wa Masuala ya
Ulinzi wa Ikulu ya Marekani, Gayle Smith alisema Obama anakwenda
Tanzania kwa sababu nchi hiyo ni rafiki mkuu wa Marekani Afrika
Mashariki. Alisema Afrika hususan Tanzania, ni moja ya masoko muhimu
yanayoibukia ulimwenguni na Marekani lazima iongeze harakati zake barani
humo.
No comments:
Post a Comment