Pemba: Chama cha UDP Zanzibar kimeitaka Serikali kutowalipa posho wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kuwapunguzia mshahara wajumbe ambao hawachangiikatia vikao vya baraza hilo.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu wa UDP Zanzibar, Juma Khamis Faki wakati akizungumza na gazeti hili baada ya kubaini kuna baadhi ya wajumbe wa baraza ambao kazi yao ni kusinzia wakati wakiwa barazani .
Alisema kutolipwa posho kwa wajumbe hao pamoja na
kukatwa kwa mishahara yao itakuwa ni fundisho kwa wale wasio na kawaida
ya kuchangia hoja pamoja na kuwatetea wananchi
waliowachagua .
Alibainisha kuwa vitendo vya viongozi hao wa
majimbo kushindwa kuchangia hoja kwenye vikao hivyo kumesababisha baadhi
ya majimbo kuwa nyuma kimaendeleo hasa majimbo ya uchaguzi ya
Pemba,licha ya ahadi walizoombea kura .
“Ni vyema Serikali kuwa na utaratibu wa kutowalipa
posho ya kikao pamoja na kuwakata mishahara wajumbe ambao kazi yao ni
kusinzia wakiwa barazani, kwani wamekuwa wakitafuna fedha za umma bila
ya kuzifanyia kazi,” alishauri mwanasiasa huyo.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika majimbo ya
uchaguzi ya Kisiwa cha Pemba wanatoka CUF kwa kushirikiana na CCM
wanaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Kumekuwapo na malalamiko ya mara kwa mara katika
mihimili yote miwili ya Bunge na Baraza la Wawakilishi, kwa baadhi yao
kulala wakati wa vipindi vya majadiliano vikiendelea na kushindwa
kuwakilisha matatizo ya wananchi wao.
No comments:
Post a Comment