Nukuu muhimu za Rais Barack Obama
WAKATI tukijiandaa kumpokea Rais Barrack Obama wa Marekani anayetarajiwa kuwasili nchini wiki ijayo ni vyema kujikumbusha nukuu muhimu alizowahi kusema.
Ni muda wa kubadilisha mfumo wetu wa kufanya biashara hapa Washington ili kujenga misingi mipya kwa karne ya 21. Tunahitaji kufanya mabadiliko serikalini kuongeza ufanisi, uwazi na ubunifu. Hili linahitaji watu wanaofikiri kwa umakini na kuhakikisha kila senti (dola) inayopatikana inatumika vizuri.
Barrack Obama
Nina watoto wawili. Mmoja wa miaka tisa na mwingine miaka sita. Hawa ninawafundisha kuhusu suala la maadili. Lakini kama watafanya kosa sitaki waadhibiwe na mtoto. Kama watu hawawezi kuamini Serikali yao namna inavyofanyakazi, kuwalinda na kutetea maslahi yao ni vigumu. Barrack Obama
Ninaamini kuwa ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke, hivyo siungi mkono ndoa za ushoga. Lakini unapoangalia Katiba ya nchi kuhusu haki za watu ni jambo jingine. Katiba yetu imepanua wigo wa haki za watu na huwezi kuzipuuza. Barrack Obama
Nimepita milima na mabonde kufika hapa nilipo, lakini huu ni mwanzo tu. Leo hii tunaanza safari mpya ya kuhakikisha duniani tunayoishi inakuwa mahali salama zaidi kwa watoto wetu kuliko ilivyokuwa jana. Barrack Obama
Niseme tu bila kutafuna maneno kuwa kuwa mama yangu alikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa mstari wa mbele kwenda kanisani kila wiki, lakini hakuwahi kunipeleka kanisani. Hata hivyo, mimi ni Mkristo ninayeamini kuwa Mungu ni muweza wa yote.
Barrack Obama
No comments:
Post a Comment