TTCL

EQUITY

Friday, June 28, 2013

Mbunge ataka Idara ya Uvuvi iondolewe

 

Dodoma
MBUNGE wa Mafia, Abdulkarim Shah (CCM), ameitaka Serikali kuiondoa Idara ya Uvuvi kwenye Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Shah alitoa kauli hiyo bungeni mjini hapa jana, alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa wizara hiyo, ambapo alitaka ihamishiwe Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mbunge huyo alisema kuwa watendaji wa idara hiyo hawafanyi kazi inavyopaswa, hivyo mapato yatokanayo na zao hilo hayaridhishi.
“Mheshimwa naibu waziri, kwanini usiiondoe Idara ya Mifugo na kuihamishia Wizara ya Utalii kwani wameshindwa kuleta tija,”aliuliza Shaha.
Akijibu swali hilo, Waziri wa wizara hiyo, Dk. David Mathayo, alisema idara hiyo haitengewi fedha hivyo inashindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Dk. Mathayo alisema hata hivyo, suala la kupanga idara ni la Rais Jakaya Kikwete, hivyo hawezi kufanya hivyo.
Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa Kwela, Ignas Malocha (CCM), alitaka kujua sababu zinazosababisha kuwepo kwa uhaba wa samaki katika Ziwa Rukwa.
Sanjari na hilo, mbunge huyo pia alitaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhakikisha ziwa hilo linapata samaki kama ilivyokuwa kipindi cha zamani kuhakikisha kipato kwa wananchi wazungukao.

No comments:

Post a Comment