Kiwanda cha mafuta Mombasa hatarini
Wauzaji petroli
wameitaka serikali ya Kenya kufuta sheria inayowalazimu kununua nusu ya
mafuta kutoka kiwanda kilichopo Mombasa.
Ishara zote sasa zinaonyesha
kiwanda cha kusafisha mafuta ya petroli cha Kenya huenda kikafungwa.
Wauzaji mafuta ya petroli wameitaka serikali ya Kenya kufuta sheria
inayowalazimu kununua takriban nusu ya mafuta kutoka kiwanda hicho
kilichopo Mombasa.
Je, haya yanamaanisha Kenya huenda ikakosa fursa
ya kukuza uwezo wake wa kiuchumi kutokana na kusafisha mafuta, endapo
itafunga kiwanda hicho cha kipekee Afrika Mashariki? Anne Soy anaripoti.
No comments:
Post a Comment