MPE MTOTO NAFASI..
Watoto wakionesha ufanisi wao wa sanaa ya maigizo yaliyo ambatana na ngoma za utamaduni Jijini
Bujumbura Nchini Burundi katika siku ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyo fanyika hivi karibuni.
watoto kama hawa wakipewa fursa ya kuonesha vipaji vyao vinaweza kuwasaidia kwa siku za baadaye katika maisha yao, lakini wazazi wengi Barani Afrika hawajui kuendeleza na hatakutambua vipaji vya watoto wao na kuvigeuza kuwa msaada katika maisha yao tofauti na nchi za mabara mengine kama nchi ya India, China Marekani, Uingereza pamoja na nyingine ambapo wazazi wengi wamewapa watoto wao nafasi za kutambua vipaji vyao na kuviendeleza katika sanaa mbalimbali na hasa katika mambo ya teknolojia na mfano mzuri ni kijana mwenye umri wa miaka 17 aliyeshangaza dunia kwa kubuni programu ya kutumika katika simu za mkononi ameweza kuwa milionea akiwa ni mwenye umri mdogo baadaya kuuza programu aliyo itengeneza pekeyake. lakini tujiulize swali moja barani afrika vijana wenye umri wa miaka 17 au hata 20 wanapewa fursa za kutumia vifaa kama kompyuta kwa kiwango gani.
Hizi ni changamoto kwa walezi na wazazi barani afrika katika kutambua na kuendeleza vipaji vya watoto badala ya kuwapeleka shule na kuwapa elimu bila malengo mbadala katika maisha yao, kwa upande wa sanaa kama muziki na maigizo tumejitahidi kidogo sana lakini kuna mamboa au michezo mingine ambayo viongozi walio pewa ridhaa ya kusimamia na kuendeleza mambo mbalimbali wamepuuza na kuona hayana mantiki katika taifa lakini nchi kama China na India wamechukuwa na kuyafanya ni ajira na pia ni njia mojawapo ya kukuza uchumi wa nchi zao.
No comments:
Post a Comment