JINSI YA KUISHI NA WATU WENYE TABIA NGUMU (HOW TO DEAL WITH DIFFICULT PEOPLE) (Jielewe wewe na uwaelewe wengine pia)
4. Unafanya nini
unapopingwa? (what do you do when you are critized)
Wako watu wanaopendelea kupinga wengine
katika kila kitu, hata katika vile visivyostahili kupingwa,hakuna chochote
chema kinachoweza kusemwa na yeyote, bali yeye peke yake. Hata kama kilichosemwa
kina ukweli kwa asilimia kubwa basi mtu huyu atajitahidi walau kurekebisha hata
lugha tu, ili mradi kisipite hivihivi bila yeye kukipinga japo kidogo (hawa
ndio wale wenye tabia ngumu). Hali hii huwapa kufurahi na kujijengea nguvu kwa
jinsi wanavyopinga wengine. Ni kweli upinzani mwingine ni wa ukweli
na unajenga lakini hapa nakazia wale wanaopinga ili tu kujifurahisha nafsi zao
na kuwafanya wale wanaowapinga waumie mioyo. Je unapopigwa, unajibuje? Je unajitetea
au unajishusha na kukubali kila kinachopingwa kwa kuamini kuona anayepinga yuko
sawa na kwa hiyo unayameza maoni yako yote, bila kuchambua kwa kina mapingamizi
hayo. Kunajinsi ambavyo unaweza kumkabili au
kumjibu anayekupinga na ikawa kama umeweka petroli kwenye moto, upinzani
utawaka na hata kuleta magovi, lakini pia aiko njia ambayo unaweza kumjibu mtu
huyu na ukanyamazisha fukuto lote.
5. Je unamtazamo hasi
(mtazamo usiofaa) na wa kudumu katika kitu fulani? Mfano; Labda unasema “mambo
yangu hayaendelei tangu nihamie katika nyumba hii au “Mambo yangu yanakwama
tangu nimuoe au niolewe na huyu” “Ni matatizo tu tangu tuoane” “Watoto hawa
hasara tu.” n.k. Mtazamo huu hasi, waweza kukugharimu sio tu kukunyima raha
bali pia waweza kuharibu hisia zako na za wengine pia. Ukijikuta katika hali
hii ni vema kujifahamu na kujitahidi kuelewa nini tatizo husika na jitahidi
kubadilisha mtazamo wako. Tafuta vile vitu ambavyo unaweza kuvitazam katika
mtazamo chanya hata kama ni vidogo. Tafuta kuviongelea vile unavyovipenda zaidi
ya vile usivyovipenda.
6. Je unazimeza hisia
zako zote, zilizo nzuri na zilizo mbaya? Je unaona ni ngumu sana kusema
“nakupenda” “umependeza” “umeniudhi” n.k. labda unaweza kusema neno
moja tu na siyo lingine. Wengi wetu tumekuzwa katika mazingira
ambayo tunahofu kusema chochote ili tu tusije tukamkwaza mtu, hata kama
tunaumizwa au tunajisikia vema kusema kitu fulani, lakini tunajizuia. Na badala
yake tunakwenda kusemea pembeni. Yamkini kunyamza kunaweza kuwa kwa faida
katika baadhi ya mazingira lakini sio hata katika kukubali vitu visivyofaa.
Hakuna ubaya wowote katika kuelezea jinsi unavyojisikia moyoni mwako ili mradi
tu unaeeleza kila unachokihisi kwa hali njema na sio kwa hasira au shari.
Katika hali hii kamwe hutowapoteza marafiki zako, na kama kuna yoyote aliye
rafiki atasumbuliwa na hili basi usihofu, kubali tu kumpoteza kwa kuwa hakuwa
wa muhimu au wa msaada sana kwako.
Hali ya kujifanya hujaumia au
hujakwazika na wakati umekwazika na unalia ndani kwa ndani inaumiza na kufanya
ujisikie vibaya sana. Inakufanya uzidishe mazingira ya msongo wa mawazo
(stress) hasa pale unapojiwazia wewe mwenyewe zaidi ya kushuhulika na wale
waliokuudhi. Mtazamo wako jinsi unavyojiona wewe mwenyewe huathirika sana, na
pia waweza kujisababishia tatizo hasa pale wale wenye tabia ngumu watakapo kugundua
kuwa huwezi kusema chochote hata ukiumizwa na hii itawafanya wakugeuze mpira wa
kuchezea.
7. Je Wewe ni kati ya
wale wanaojiamini kusema chochote wanachokifikiri bila kujali matokeo yake? Hembu fikiri jinsi unavyojisikia pale ambapo mtu au watu wengine
wangefanya hivyo hivyo kwako. Je unataka kuwasababishia wengine maumivu ya
moyoni? Kusema chochote kinachoshuka toka kichwani mwako kupitia kinywani mwako
bila kufikiri juu ya matokeo au athari zake kwa wale wanaokusilikza au
waliokuzunguka kwaweza kukupotezea marafiki na kuishusha hadhi yako kwa urahisi
sana. Mara nyingi mtu wa jinsi hii huweza kujikuta akiwa pweke na anayepingana
na ulimwengu (kila mtu anamchukia), hii ni kati ya hisia za kuhuzunisha na
kuumiza sana muda wote, lakini pia huumiza zaidi pale unapogungua kuwa ni
maumivu uliyojitakia mwenyewe. Peke yako unajikuta umetegwa na mtego wa kihisia
na kukuzamisha usipoweza kujikwamua tena.
na mtaalamu wetu wa saikolojia Bw. Chris Mauki
No comments:
Post a Comment