TTCL

EQUITY

Tuesday, February 7, 2017

MWIGULU NCHEMBA ATOA UFAFANUZI WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUSINDIKIZWA NA VING'ORA

WAKUU wa Mikoa na Wilaya ni ruksa kutembea na magari ya polisi yenye ving’ora wanapokwenda kwenye shughuli mbalimbali za utendaji, zikiwamo za ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Ufafanuzi huo ulitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliyetaka kujua kama ni itifaki za kiserikali kwa wakuu wa mikoa na wilaya kutembea na magari ya polisi yenye ving’ora.
Mbowe alishangaa na kuhoji kuwa ni itifaki gani kwa viongozi hao, akatoa mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutembea na kikosi cha polisi chenye watu tisa, pikipiki za polisi za kuongoza msafara na gari lenye king’ora.
Waziri Mwigulu alisema, viongozi hao hawaruhusiwi kutembea na misafara yenye magari ya polisi yenye ving’ora wanapokwenda ofisini, labda kama viongozi wa mkoa na polisi wapo ofisi moja, lakini hawakatazwi kwenda navyo wanapoenda eneo la kazi maalumu.
“Viongozi hao wanapokuwa na majukumu ya kwenda kutoa maelekezo au kufanya shughuli zinazohusiana na majukumu ya ulinzi wa maeneo yao, wanaruhiswa kuwa na magari hayo,” alisema.

No comments:

Post a Comment