TTCL

EQUITY

Monday, March 9, 2015

Jinsi Ya Kufufua Mafaili Yaliyofutwa Katika Simu/Kompyuta!

Asoftech ni programu ya kuzifufua data zilizofutwa ambayo ni ya bure kushusha na rahisi kutumia na pia ina ukubwa mdogo  (kama 4MB hivi) kwa msaada wa hii programu (software) utafufua mafaili yaliyofutwa kwenye vifaa vya uhifadhi wa data mbalimbali kama vile ‘pen drive, USB drive, external Hard Drive, memory card’ na sehemu zingine.

Inabidi kuacha kutumia mafaili katika simu yako mara tuu unapotaka kufufua mafaili yaliyofutika katika SD Card  kwa sababu haitawezekana kufufua mafaili wakati mafaili mengine yanatumika muda huohuo katika simu.
Kitu kingine cha kuweka akilini ni kwamba hautawezekana kufufua mafaili kwa kutumia Asoftech kama utakua umefomati (Format) SD Card/Hard Drive  ya kifaa chako.
FUATA NJIA HIZI KUFUFUA MAFAILI HAYO
1. Kwanza kabisa inabidi uishushe hiyo programu (Software) ya Asoftech hapa 
2. Baada ya kuishusha (download) fanya mpango wa kuipakua (install)….. itakuchukua muda kidogo tuu
3. Kutumia Asoftech inakubidi uwe ‘Administrator’ katika kompyuta yako, kama ni Admin nenda mpaka kwenye icon ya Asoftech ‘ Right Click’ kisha bofya ‘Run As Administrator‘.
4. Baada ya hapo unganisha simu yako au kifaa kingine katika kompyuta yako. Hakikisha kompyuta yako inasoma memori kadi ya simu yako. Au kama unaweza toa memori kadi ya simu weka katika sehemu ya kusoma kadi (card reader)na uunganishe katika kompyuta. Kama unataka fufua mafaili katika Hard Disk Drive ya kompyuta yako unaweza ruka hatua hii.
5. CHAGUA Diski Uhifadhi (DRIVE)
recover-deleted-files-from-sd-card-select-drive
Chagua Drive
Hatua ya hapo juu ikipita na Asoftech ikifunguka zitatoka orodha ya diski uhifadhi kibao, chagua moja ambayo unataka kufufua data zake. Chagua drive ya Sd card au Hard drive nyingine na kisha bofya NEXT
6. Itaanza fanya uchambuzi katika diski/ SD card yoyote uliyoichagua. Uchambuzi ukishakamilika itatoa orodha ya mafaili mengine na maelezo ya aina zake (kama vile mp3 au .jpg na zingine)
7. FUFUA MAFAILI
recover-deleted-files-from-sd-card-recover
Fufua Mafaili
Sasa unaweza kubonyeza “recover’ kufufua mafaili uliyo yachagua na pia unaweza kutochagua mafaili ambayo hutaki kuyafufua.
Kwa kutumia njia hii unaweza fufua aina yoyote ya faili katika  Hard Disk Drive na hata SD card.

No comments:

Post a Comment