TTCL

EQUITY

Friday, February 3, 2017

Ishu ya Madawa: Ditto Afunguka Kutajwa na Makonda sakata la madawa

Image may contain: 1 person, sitting
Mhe. Paul Makonda Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari hawapo pichana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ajilipua kwa kuwataja Wauzaji Dawa za kulevya.
Wamo pia Maofisa Tisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar Es Salaam ,wakiongozwa na Christopher Fuime ambaye alikuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni.
Makonda amuonya kamanda Sirro asema yupo tayari kufa au kupoteza nafasi ya Ukuu wa Mkoa kwa kuongea ukweli.
Makonda amewataja Askari Polisi tisa(9) ambao amewatuhumu kuwa wanashirikiana na wauza Dawa za Kulevya.
Pia Makonda amewataja wanaotuhumiwa kutumia dawa za kulevya wakiwemo wasanii TID, Wema Sepetu, Chid Benz, Recho, Babuu wa Kitaa, Hamidu, Petiti man na kuwataka waripoti Kituo cha Polisi.

Wakati huo huo watuhumiwa wengine tayari wamekamatwa wapo kituo cha Cetral. Pia amelishutumu Jeshi la polisi kushindwa kuwatambua na kuwakamata waagizaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya wakati wanajulikana hata kwa waendesha bodaboda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa taarifa hii ya uchunguzi kuhusu biashara ya dawa za kulevya jiji la Dar es salaam na kuwataja watu aliowaita watuhumiwa wa biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya.Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 2, 2017, Makonda amewataja vigogo na mastaa wanaotuhumiwa kutumia madawa ya kulevya wakiwemo Askari Polisi 9 wanaotuhumiwa kuhusika na biashara hiyo. Wengine wanaotuhumiwa kutumiwa dawa za kulevya ni mastaa wa filamu na muziki na wametakiwa kuripoti kesho kituo cha Polisi Central.“Kuna maeneo watu wanatuambia madawa ya kulevya wanayapata sehemu hizo, wamiliki wake kesho niwakute polisi, wasipokuja nitawafuata… kama unajua una eneo unafanya biashara za dawa za kulevya Dar es salaam natoa siku 7 biashara hii iishe, operesheni hii naiongoza mwenyewe. Kama Kamishna Sirro na timu yake watashindwa kutokomeza dawa za kulevya Dar es salaam maana yake wamekosa sifa za kuendelea kuwa askari” amesema Makonda.Makonda amezitaka mamlaka za kijeshi kuwaweka chini ya ulinzi askari hao kwa mamlaka yake ili waweze kutoa taarifa kwanini dawa za kulevya bado zinaendelea kuwepo.Aidha, Makonda ametaja baadhi ya maeneo ambayo Wamiliki wake wamepewa vibali vya kufanya biashara lakini wanatumia maeneo hayo kinyume na masharti ya biashara kwa kuuza dawa ya kulevya ambapo amewataka kufika kituo kikuu cha polisi kesho saa tano na wasipofanya hivyo atawafata mwenyewe.
Wakati huohuo Msanii wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Moyo Sukuma Damu’, Lameck Ditto amefunguka na kusema yeye hahusiki na biashara ya dawa za kulevya wala matumizi ya dawa za kulevya na kusema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikosea kutaja jina.
Ditto amefunguka na kusema kuwa hata yeye alisikia jina lake likitajwa kwenye kundi la wasanii ambao wanahitajika kufika kesho kituo cha polisi na kusema anadhani kuwa Mkuu wa Mkoa alikosea kutaja jina lake.
“Kiukweli mimi mwenyewe nimeshtuka sana maana sijihusishi kwa namna yoyote na madawa ya kulevya, siuzi wala kutumia na siku zote nayapiga vita sababu natambua si mazuri katika jamii.
“Nadhani Mheshimiwa alikosea kutaja jina maana alisema Ditto lakini baadaye niliona amerekebisha na kusema Titto, hivyo naomba Watanzania watambue mimi sihusiki na madawa ya kulevya” alisema Lameck Ditto.

Babuu wa Kitaa akiwasili Kituo Kikuu cha Polisi majira ya saa 4: 38


T.I.D naye akiwasili kituoni hapo saa 5:07 asubuhi.


Hamidu Chambuso aka ‘Nyandu Toz’ akiwasili kituoni majira ya saa 5: 38.
 
Wanahabari wakichukua matukio kituoni hapo.

Mwingine ambaye mpaka sasa ameshawasili ni Mmiliki wa Klabu ya Usiku ya Element aliyewasili majira ya saa 5.00 akiambatana na mawakili wake wawili.

wema Sepetu akitoka kuchukuliwa maelezo mara baada ya kuitika wito wa kisheria

No comments:

Post a Comment