Waislamu 200 wanaofanya kazi katika kiwanda kimoja cha nyama Colorado, Marekani wamefutwa kazi baada yao kugoma.
Walikuwa wamegoma kulalamikia kunyimwa uhuru wa kuswali wakiwa kazini.
Wengi wao ni wahamiaji kutoka Somalia.
Msemaji
wa Baraza la Uhusiano wa Wamarekani na Waislamu Jaylani Hussein anasema
wafanyakazi hao katika kiwanda cha Cargill Meat Solutions walikuwa kwa
muda mrefu wameruhusiwa kuswali.
Msemaji wa kiwanda hicho cha
Cargill alisema kuna uhuru wa kuabudu kiwandani lakini lazima mahitaji
ya kuabudu yaambatane na mahitaji ya kazi kiwandani.
Mkurugenzi
mkuu wa Tume ya Haki za Kibinadamu Somalia Omar Jamal, amesema mameneja
wanafaa kufahamu kwamba Waislamu huhitajika kuswali mara kadha kwa siku,
hili likitegemea kipindi cha mwaka.
No comments:
Post a Comment