Kuna malalamiko mengi tumekuwa tukiyasikia kuhusu Ikulu za nchi kuhusishwa na ufujaji mkubwa ama matumizi mabaya ya fedha.
Hizi ni picha na orodha ya Ikulu kumi zinazoongoza kugharimu pesa nyingi kuanzia kwenye ujenzi mpaka matumizi yake ya kila siku.
No. 1- Jumba jipya la Ikulu ya Uturuki, liko katika jiji la Ankara na kwa sasa huenda likawa jumba kubwa zaidi kuliko Ikulu ya Marekani. Ujenzi wake umegharimu zaidi ya Dola Mil. 350.
No.2- White House, Ikulu ya Marekani. Ikulu hii iko Washington D.C, na imekuwa ikitumika kama Ikulu tangu mwaka 1800, Marekani ikiongozwa na rais John Adams.
No. 3- Planalto, Ikulu ya rais wa Brazil. Iko katika jiji la Brasilia. Imekuwa ikitumika kama Ikulu tangu mwaka 1960, wakati huo rais akiwa Oscar Niemeyer.
No. 4- Grand Kremlin, Ikulu ya Urusi iliyopo jijini Moscow. Imeanza kutumika kama Ikulu tangu mwaka 1849.
No. 5- Jumba la Ikulu ya Taipei, Taiwan. Imekuwa ikitumika kama Ikulu tangu mwaka 1950.
No. 6- Casa Rosada, Hii ni Ikulu ya Argentina. Ipo katika jiji la Buenos Aires.
No. 7- Hanoi, hii ni Ikulu ya Vietnam. Iko katika jiji la Hanoi.
No. 8- Hii ni himaya ya Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ipo katika jiji la Kinshasa.
No.9- Hii ni Ikulu ya Korea Kusini, inaitwa Park Geun-hye. Iko katika jiji la Seoul.
No. 10- Inafahamika kama Schloss Bellevue, ni Ikulu ya Ujerumani. Iko katika jiji la Berlin.
No comments:
Post a Comment