TTCL

EQUITY

Wednesday, January 13, 2016

WAALIMU WASTAAFU DODOMA WAOMBA KUPATIWA MAFAO YAO

 
Baadhi ya walimu wastaafu mkoani Dodoma wameiomba serikali ya awamu ya tano kuharakisha malipo ya mafao yao yaliyodumu kwa miezi kadhaa sasa ili kuwapunguzia ukali wa maisha.

Wameyaeleza hayo wakati wa kipongezwa na Chama cha walimu mkoa wa Dodoma   kwa utumishi wao uliotukuka ndani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 15.

 Akikabidhi zawadi kwa wastafu hao mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Dodoma Samsoni Mkotya amesema Baraza la chama hicho taifa limendelea kutenga   fedha kwa ajili ya  kutoa mkono wa pongezi pindi wanachama wanapomaliza utumishi wao.

Zawadi zilizokabidhiwa kwa wastafuu hao wane ni pamoja na Bati 80 zenye thamani ya shilingi Milioni moja  laki sita na elfu sitini  ambapo kila mmoja amepewa bati 20.

No comments:

Post a Comment