TTCL

EQUITY

Wednesday, January 13, 2016

MBUNGE WA RUVUMA BI. JACKLINE NGONYANI AMEWATEEMBELEA WAATHIRIKA WA MAAFA YA MVUA

Baada  ya wilaya za Mbinga  na Songea  vijijini kukumbwa na maafa ya mvua ambapo familia kadhaa zilikosa mahali pa kuishi  baada ya nyumba zao kubomoka na kuezuliwa  na mvua,  maafa hayo yameikumba wilaya ya Songea mjini baada ya nyumba ishirini  kuezuliwa na kubomolewa na mvua katika  mtaa wa Ruvuma juu mjini Songea mkoani  Ruvuma.

Mwenyekiti wa mtaa wa Ruvuma juu katika manispaa ya Songea Bi. Ester Nchimbi ameeleza zaidi kuhusiana na maafa hayo ya mvua yaliyoezua na kubomoa nyumba ishirini na kuziacha familia ishirini zikiwa hazina mahali pa kuishi.

Kutokana na majanga hayo mbunge wa viti maalumu wa mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Jackline Ngonyani Msongozi amewatembelea waathirika wa majanga hayo na kuwapatia mabati mia moja huku waathirika wa majanga hayo wakishukuru kwa msaada huo.

No comments:

Post a Comment