Maveterani wa Umoja wa
Vijana wa Young Pioneers wakipiga makofi wakati wa kuingia mgeni rasmin
Mhe Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya
hiyo kuendeleza Vijana Zanzibar.
Maveterani wa Umoja wa
Vijana wa Young Pioneers wakipiga makofi wakati wa kuingia mgeni rasmin
Mhe Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya
hiyo kuendeleza Vijana Zanzibar.
Ustaadhi akisoma Quran
kabla ya Uzinduzi huo wa Jumuiya ya Veterani wa Umoja wa Vijana wa Young
Pioneers uliofanyika katika ukumbi wa ZSSF kiwanja cha Watoto Kariakoo
Zanzibar.
Maveterani wa Young Pioneers wa Umoja wa Vijna wakimsikiliza msoma Quraan wakati wa uzinduzi huo.
Katibu wa Veterani wa Young
Pioneers, Said Shaban akitoa maelezo ya Jumuiya hiyo ya Veterani wa
Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakati wa Uzinduzi wake uliofanyika
katika Ukumbi ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.

Mjumbe
wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Veterani wa Young Pioneers, Mhe.
Khadija Hassan Aboud akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa
Jumuiya hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya
Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Mhe Asha Ali
Abdallah akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya ya
Veterani ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers, katika Ukumbi wa ZSSF
Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Waziri wa Fedha Zanzibar
Mhe Omar Yussuf Mzee akiwahutubia Veterani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana
wa Young Pioneers wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika
Ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. na kutangaza Fedha
zilizopatika katika harambee aliyoiazisha kwa ajili ya kukuza Mfuko wa
Jumuiya hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 9,724,000/= zimepatika ikiwa
Fedha Taslimu Shs 3.874,500 na Ahadi Shs.5,850,000/=
Wanachama wa Jumuiya ya Veterani wa Young Pioneers wakimsikiliza mgeni rasmi akiwahutubia wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya yao.
Veterani wa Jumuiya ya
Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakimsikiliza mgeni rasmi wakati
akiwahutubia na kuwazindulia Jumuiya yao.
Wazee Maveterani wa Young
Pioneers wakiwa meza kuu wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe Omar Yussuf Mzee
akiwahutubia wakati wa uzinduzi huo wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika
Ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Maveterani wakichangia katika harambee hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo.
Maveterani wakichangia katika harambee hiyo ya uzinduzi wa Jumuiya hiyo.
Veterani wa Umoja wa Vijana
aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Tanzania Mhe Sukwa Said
Sukwa akichangia katika harambee hiyo, ya uzinduzi wa Jumuiya hiyo.
Veterani
wa Young Pioneers Mhe. Aboud Talib Aboud akichangia jambo wakati wa
uzinduzi wa Jumuiya hiyo. baada ya kuitishwa upato wa maridadi na
kupatikana shilingi milioni 9,724,000/= papo kwa papo wakati wa harambe
hiyo ya Veterani wa Young Pioneers.
Veterani wa Young Pioneers
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis akichangia
wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Jumuiya
ya Veterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers Meja Generali Mstaaf
Hassan Vuai Chema, akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Waziri wa
Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee baada ya kuwazinduliwa Jumuiya yao
katika ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Veterani wa Young Pioneers
Makame Haji Makame (Cairo) akihamasisha kwa kuimba wimbo wa Vijana
wakati huo wa kuhamasisha vijana katika kujenga taifa katika uzinduzi wa
Jumuiya hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa watoto kariakoo
Zanzibar, kabla ya kuanza kwa kongamano la Jumuiya hiyo
Mwenyekiti wa Kongamano
hilo la Veterani wa Young Pioneers, Mhe Aboud Talib Aboud akiongoza
kongamano hilo kuzungumzia kumkomboa kijana katika kujiajiri na
kujiengezea kipato na kuwa na maadili mazuri.

Mtoa Mada katika Kongamano
hilo la Uzinduzi wa Jumuiya ya Maveterani ya Young Pioneers Association
Ndg Ali Khamis akitoa mada kuhusu Wajibu kwa Kijana, kwa wajumbe wa
mkutano huo wa uzinduzi uliofanyika ukumbi wa kiwanja cha watoto
kariakoo Zanzibar.
Veterani wa Young Pioneers wakimsikiliza mtoa mada juu ya Maendeleo ya Vijana katika kujikomboa kiuchumi.
Veterani wa Young Pioneers wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakato wa Kongamano.
Mgeni rasmi Mhe Omar Yussuf
Mzee akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Veterani wa
Umoja wa Vijana Young Pioneers wa wakati huo wa Umoja wa Vijana
Zanzibar. Baada ya Kuizindua Jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment