Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa amewataka
wafugaji mkoani humo kuuza mifugo yao ili kuweza kukabiliana na tatizo
la njaa linaloukabili mkoa huo kwa sasa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Luteni Chiku Gallawa
Gallawa
ametoa wito huo wakati akizungumza na East Africa Radio kwa njia ya
simu, kuhusiana na hatua zinazochukuliwa na serikali ya mkoa wa Dodoma
katika kukabiliana na tatizo la njaa lililozikumba baadhi ya Wilaya
mkoani humo.
Aidha mkuu huyo anaeleza kuwa kuna tani za chakula ambazo zimetengwa
kwa ajili ya kuwanusuru wananchi wanaokabiliwa na tatizo hilo.
Baadhi ya wilaya za mkoa wa Dodoma ikiwemo Kondoa, Bahi na Mpwapwa
zinakabiliwa na baa la njaa hali iliyowapelekea kuwalazimu wakazi hao
kula matunda pori ili kuweza kunusuru uhai wao.
No comments:
Post a Comment