Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu wa
wizara mbalimbali na kuwasainisha kiapo cha utii na uaminifu leo Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya kusomewa hati ya utii mbele ya kamishna wa tume ya
maadili Rais Dkt. Magufuli aliwataka makatibu wakuu na manaibu hao kama
kuna ambaye hajaridhia masharti ya kiapo hicho basi akae pembeni.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania amewataka Makatibu wakuu hao
wajue kiapo hicho kinamaanisha wameridhia jukumu la kuwatumikia wananchi
katika maendeleo huku akisema kuwa utaratibu huo wa kula kiapo cha utii
utaendelea kwa viongozi wengine wateule wakiwemo wakuu wa mikoa na
wilaya.
Mh. Majaliwa ameongeza kuwa mipango yote ya maendeleo inaanzia kwa
makatibu wakuu ambao wana jukumu la kuhakikisha maendeleo yanawafikia
wananchi huku wakipata usimamizi wa wakuu wa wilaya na mikoa.
No comments:
Post a Comment