Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa -TAMISEMI, GEORGE SIMBA CHAWENE amewavua madaraka
Mkurugenzi wa Manispaa ya DODOMA, AUGUSTINE KALINGA na Afisa Elimu Vifaa
na takwimu katika manispaa hiyo JOSEPHINE AKIM kwa kushindwa kusimamia
maelekezo ya serikali ya kutoa elimu bure.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, George Simba Chawene.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini DODOMA, Waziri
SIMBACHAWENE amesema uamuzi huo umefuatia viongozi hao kuandika waraka
unaoelekeza wakuu wa shule katika Manispaa hiyo kuchangisha fedha kutoka
kwa wanafunzi.
Amesema Afisa Elimu Msingi wa Manispaa hiyo SCHOLA KAPINGA amepewa
onyo kali kwa kuanza kutekeleza waraka huo unaopingana na maelekezo ya
Rais JOHN MAGUFULI.
No comments:
Post a Comment