TTCL

EQUITY

Monday, January 25, 2016

Kesi ya kupinga ubomoaji Kinondoni yaahirishwa


KESI ya kupinga bomoabomoa iliyotarajiwa kutolewa maamuzi leo jijini Dar es Salaam katika Mahakama Kuu kitengo cha ardhi imeahirishwa tena,  badala yake hukumu itatolewa  Januari 26, 2016 siku ya jumanne .
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulya, (CUF) ambayo inataka wananchi hao mbali na kubomolewa wapewe maeneo mbadala na yenye usalama ambapo wakili wa upande wa mlalamikaji akiwa ni Abubakar Salim aliyewataka wananchi waliokuwa nje ya mahakama hiyo kutochoka kuendelea kufuatilia kesi hiyo.

 
Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi jijini DAR ES SALAAM imeahirisha kesi ya kupinga ubomoaji wa nyumba za wakazi 681 wa kata tatu za Halmashauri ya Manispaa ya KINONDONI zinazodaiwa kujengwa katika maeneo oevu na ya wazi
Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi jijini DAR ES SALAAM imeahirisha kesi ya kupinga ubomoaji wa nyumba za wakazi 681 wa kata tatu za Halmashauri ya Manispaa ya KINONDONI zinazodaiwa kujengwa katika maeneo oevu na ya wazi.

 1.Wakili wa walalamikaji anayesikiliza kesi hiyo akihojiwa na wanahabri baada ya kuwapa taarifa wakazi waliobomolewa Nyumba zao za mabondeni kuwa kesi hiyo itasikilizwa hapo kesho. 
 wakili anayewawakilisha wakazi hao Abubakar Salim.
Akizungumza nje ya jengo la Mahakama ya Ardhi, wakili anayewawakilisha wakazi hao ABUBAKAR SALIM amesema uamuzi huo umefikiwa na jaji PANTERINE KENTE kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya vielelezo juu ya kesi hiyo.
Aidha wakili SALIM amewataka wakazi hao kuwa watulivu wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama.
Zoezi la bomoa bomoa limeendelea kufanyika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kubomoa nyumba zilizojengwa maeneo oevu, ya wazi na mabondeni.

3.Baadhi ya wananchi walofika mahakama hapo wakiwa nje ya maduka yaliyopo nje ya mahakama hiyo. Wakili wa mlalamikaji anayesikiliza kesi hiyo, Abubakar Salim, akihojiwa na wanahabari baada ya kutoa taarifa kwa wakazi waliobomolewa nyumba zao mabondeni waliokuwa wamejitokeza kusikiliza kesi ambayo maamuzi yake yatatolewa jumanne 26 januari 2016.

2.Wananchi wakimsikiliza wakili huyo juu ya kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi hapo kesho.Baadhi ya wananchi waliofika mahakamani  hapo wakimsikiliza wakili Salim (hayuko pichani).

No comments:

Post a Comment