TTCL

EQUITY

Wednesday, January 13, 2016

MGODI WA NORTH MARA SERIKALI YAIPA WIKI MBILI KUJA NA MAJIBU YA RIPOTI YA MAJI

Serikali imetoa wiki mbili kwa baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini kuchukua sampuli za maji yanayotiririka kutoka mgodi wa North Mara na kutoa hadharani matokeo uchunguzi wake ikiwa njia moja wapo ya kumaliza kabisa kilio cha miaka zaidi ya kumi kuhusu madai ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo kuwa   maji hayo yamekuwa yakisabisha madhara makubwa kwa binadamu vikiwemo vifo vya watu, mifugo na kuathiri vyanzo vya maji katika maeneo hayo.

Naibu waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa rais, muungano na mazingiraMh Luhaga Mpina, ametoa agizo hilo baada ya kutembelea maeneo yote ya mgodi wa North Mara ikiwa pamoja na kukagua mabwawa makubwayanayotumika kuhifadhi mabaki ya maji kutoka  mgodi huo kasha kuzungumza na uongozi wa mgodi pamoja na viongozi mbalimbali ngazi ya wilaya, kata na vijiji kumi moja vinazunguka mgodihuo.
  
Katika taarifa yake kwa naibu waziri huyo wa nchi, ofisi ya makamu wa rais, muungango na mazingira, meneja mkuu wa mgodi huo Bw Gary Chapman, amesema pamoja na madai hayo ya wananchi lakini mgodi wake ni miongoni mwa migodi nchini unaozingatia kwa kiasi kikubwa   uhifadhi wa mazingira hata kufikia hatua ya kupewa tuzo mbalimbali za kutoka mamlaka zinazojihusisha na uhifadhi wa mazingira.
 
Naye mkuu wa wilaya ya Tarime Bw Groriuosluoga, akizungumza mbele ya viongozi hao wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo, amemuomba kiongozi huyo kufikisha malalamiko ya fidia za nyumba zawananchi katika wizara ya nishati na madini ikiwa utekelezaji wa ahadi ya rais John Pombe Magufuli katika kumaliza kabisa migogoro ya mara kwa mara inayotokea katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment