Michezo kwa watu wenye ulemavu imefanyika hii leo
jijini Dar es Salaam, kwa kuhusisha michezo ya mpira wa kikapu,mpira wa
wavu,soka na Badminton,ikiwa ni kuhitimishwa kwa sherehe za siku ya
watu wenye ulemavu iliyofanyika kitaifa Desemba 3 mwaka huu.
Michezo
kwa watu wenye ulemavu imefanyika hii leo jijini Dar es Salaam,kwa
kuhusisha michezo ya mpira wa kikapu, mpira wa wavu, soka na
Badminton,ikiwa ni kuhitimishwa kwa sherehe za siku ya watu wenye
ulemavu iliyofanyika kitaifa Desemba 3 mwaka huu.
Afisa michezo wa Baraza la Michezo Tanzania BMT Benson Chacha, ambaye pia ni kocha wa mpira wa wavu ya walemavu amesema michezo hiyo imeonesha uwezo wa watu wenye ulemavu kuwa wanaweza kushiriki michezo na wachezaji wameonesha kiwango kizuri.
Chacha amesema changamoto kubwa inayokuwepo ni kutojitokeza kwa walemavu wengi kwenye michezo kutokana na jamii zao kuwaweka ndani na wengine wakiwa hawana mwongozo.
Naye Agnes Beny ambaye anacheza mpira wa kikapu na wavu ya walemavu amesema amefurahi kujumuika na wenzake hii leo kucheza michezo hiyo kwa kuwa imetoa nafasi kwa wenzao kushiriki kwenye michezo hiyo kwa kuwa ni mwishoni mwa wiki na wengine waliokuwa mashuleni wamepata nafasi ya kushiriki kwa siku ya Jumamosi.
Aidha Agnes ametoa wito kwa wadau na serikali kwa ujumla kuangalia michezo kwa walemavu na siyo kuegemea michezo ya watu wengine wenye viungo kamili.
Agnes amesema tatizo kubwa linalowakabili ni ukosefu wa vifaa vya kuchezea mchezo wa mpira wa kikapu ambavyo walemavu wanatumia viti vya magurudumu (wheel chair).

No comments:
Post a Comment